RAIA WA ZIMBABWE ALIYEMCHOMA MOTO USONI MWANAMKE ASHINDA KESI UINGEREZA...

Jaji ameamuru raia wa Zimbabwe ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na nusu jela baada ya kumtishia maisha mwanamke mmoja hawezi kurejeshwa nchini kwake sababu itakiuka haki zake za kibinadamu.

Muuza dawa za kulevya Valentine Harverye alimchoma moto mwathirika wake mwenye miaka 34 kwa kutumia chupa iliyochomwa ya pombe na kumbabua kwa maji yanayochemka. Alisemekana kumshambulia mbele ya watu watano au sita nyumbani kwa mwanamke huyo mwaka 2009.
Jaribio la kumrejesha kwao Harverye, lililofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani, sasa limekwama baada ya mtu huyo kukata rufani dhidi ya uamuzi huo.
Jaji wa Mahakama Kuu, Christopher Hanson alisema kumrejesha kwao Harverye mwenye miaka 22 kutakiuka haki zake za kibinadamu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuonesha utii kwa chama cha Rais Mugabe na hivyo kuweza kukabiliana na 'wakati mgumu', imeripotiwa.
Imeripotiwa uamuzi huo unaweza kukiuka Kipengele 3 cha Makubaliano ya Ulaya ya Haki za Binadamu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alisema: Tumesikitishwa na uamuzi wa Mahakama hiyo kwakuwa tunaamini kwamba raia wa nje ambao wanavunja sheria wanatakiwa kurejeshwa kwao.
"Tunachunguza taarifa za hukumu hii kabla ya kuamua kama tutakata rufaa."
Harverye  kwanza alitiwa hatiani kwa shambulio la kudhuru mwaka 2004. Aliendelea kutenda makosa mengine 12 zaidi, likiwamo shambulio hilo ambalo lilimwacha mwanamke akiwa mwenye hofu mwaka 2009.
Alihukumiwa kifungo jela kwa kosa hilo katika Mahakama Kuu ya Nottingham.
Mbunge wa Conservative Priti Patel alieleza: "Hii ni kesi ya kushitua na mfano wa kuogopesha wa jinsi mahakama kwa mara nyingine kutojali haki za mwathirika dhidi ya haki za uhalifu wa kutisha."
Mapema wiki hii ilibainishwa idadi ya wahalifu kutoka nje ambao walikwepa kurejeshwa makwao sababu 'ingekiuka haki zao za kibinadamu' imeongezeka maradufu kwa mwaka.
Takribani watuhumiwa 300 walitumia Kipengele 8 cha Makubaliano ya Ulaya ya Haki za Binadamu kuhoji haki yao ya kuishi nchini humo mwaka jana.
Takwimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani zinaonesha kwamba 'watuhumiwa 299 raia wa nje walishinda rufani zao'  mwaka jana - zaidi kutoka 177 mwaka mmoja kabla, imeripotiwa.
Kipengele 8 kinalinda haki ya ubinafsi na maisha ya familia.
Wiki moja kabla ilifichuka Sanel Sahbaz, mhalifu kutoka nje aliyefungwa jela kwa mfululizo wa mashambulio ya kutumia nguvu, alishinda kesi dhidi ya kurejeshwa kwao sababu ingekiuka haki zake za kibinadamu.
Sahbaz, raia wa Bosnia ambaye sasa anaishi huko Hertford, aliingia nchini Uingereza akiwa mtoto mwaka 1993. Tangu mwaka 2005 amefanya mlolongo wa makosa ikiwamo shambulio la kudhuru, kumiliki mali za wizi, wizi, uvunjaji wa sheria hadharani na kushambulia polisi.
Katika tukio mojawapo alimshambulia mwenye nyumba wake, akimsukuma kwenye sakafu, kumpiga mateke mara kadhaa na kumpiga chapa kichwani hadi mtu huyo alipopoteza fahamu.
Sahbaz, miaka 30, aliangukia moja kwa moja kwenye adhabu ya kurejeshwa kwao baada ya kuwa amefungwa jela miaka minne, na Wizara ya Mambo ya Ndani ikamweleza atarejeshwa kwao.
Lakini sasa ameelezwa anaweza kubaki kwa muda usiojulikana baada ya kuanzisha mapambano ya kisheria chini ya Kipengele 8.
Wanasheria wake walihoji kwamba endapo atarejeshwa kwao Bosnia atatenganishwa na wazazi wake, kaka na binamu, ambao pia wako Uingereza, jambo ambalo litakiuka haki zake.
Mnamo Februari, Waziri wa Mambo ya Ndani Theresa May alitangaza mipango ya kupitisha sheria mpya ikitaka kwamba Kipengele 8 cha Sheria hiyo kisiwe tena kikwazo kwa urejeshwaji makwao wahalifu.

No comments: