Asha Devi na mumewe, Badri Singh. |
Mama wa mwathirika wa shambulio la ubakaji Jyoti Singh Pandey amesherehekea huku za kifo zilizotolewa kwa wauaji wanne wa binti yake - akisema 'kwa sasa yuko kwenye amani'.
Asha Devi alishuhudia binti yake akitaabika kwa siku 13 hospitalini kufuatia majeraha makubwa ya ndani kwa ndani baada ya kuwa amebakwa kwa zamu ndani ya basi mjini Delhi.
Akiwa ameketi kando ya kitanda katika hospitali moja nchini Singapore, Asha, mwenye miaka 46, alimuahidi binti yake huyo mwenye miaka 23 kuwa haki itatendeka.
Mwishowe, baada ya hukumu katika mahakama maalumu, wabakaji wote wanne walihukumiwa kifo mjini Delhi Ijumaa - mwalimu wa gym Vinay Sharma, miaka 20, msafishaji basi Akshay Thakur, miaka 28, muuza matunda Pawan Gupta, miaka 19, na Mukesh Singh, miaka 26.
Ram Singh, mtuhumiwa mwenza na aliyefahamika kama kiongozi wa kundi hilo, alikutwa amekufa ndani ya selo yake mwezi Machi. Alikuwa kaka wa mtuhumiwa Mukesh Singh, ambaye aliendesha basi hilo wakati wa uhalifu huo wa kutisha.
Mtuhumiwa mdogo ambaye pia alitiwa hatiani alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu katika chuo cha kurekebisha tabia.
Mama huyo mwenye huzuni alieleza: "Hakuacha kusema matakwa yake pekee yalikuwa kuona wakinyongwa. Nafahamu matokeo haya yatamsaidia kuwa katika amani sasa."
"Maneno hayawezi kuelezea tukio hilo la kutisha. Alilia kila wakati alipozungumza kuhusiana na shambulio hilo. Kamwe siwezi kusahau jinsi shambulio hilo la kukera lilivyokuwa.
"Nakumbuka nilivyokuwa nikijaribu kumshawishi aweze kula. Lakini alikuwa katika maumivu makali mno kiasi cha kushindwa kula chakula hata kijiko cha chai.
"Alikuwa akiniambia nikae na kushika mkono wake badala yake."
Jyoti, mwanafunzi wa udaktari, alizusha mdahalo dunia nzima kuhusu matukio ya ubakaji nchini India pale aliposhambuliwa Desemba 16, mwaka jana.
Usikivu wa kimataifa uliwalazimisha majaji kuipa kipaumbele kesi hiyo - na chama cha wanasheria katika wilaya hiyo ya Saket waliripotiwa kukataa kuwatetea watuhumiwa.
Januari, Asha alifichua kwamba Jyoti alitaka waliombaka 'kuchomwa moto wakiwa hai'.
Baba Badri Singh, miaka 53, alieleza 'anajisihi kupata nafuu mno' pale jaji huyo alipowahukumu kifo kwa kunyongwa.
Alisema: "Pale jaji huyo alipotangaza hukumu ya kifo nikasonga moja kwa moja kwa wanaume hawa na nikaona hofu ya kifo machoni mwao. Wawili kati yao walikuwa wakilia.
Lakini sikujisumbua na sikuwa na sikuwaonea huruma. Sitowasamehe kamwe au kusahau walichomfanyia binti yangu. Sasa wanalipia kikamilifu walichochagua kufanya katika usiku ule."
Wanandoa hao waliongeza kwamba Jyoti alizaliwa akiwa mpambanaji, akiwa ametumia mwezi wake wa kwanza kwenye chumba cha uangalizi maalumu. Hata alipokuwa hospitalini aliamini atapambana hadi mwisho, walifafanua.
Akionesha kupigania usawa kati ya jinsia zote kwa heshima ya binti yake, Singh aliweka wazi kwamba kifo chake kimekuwa mfano wa kuvutia kwa India.
Alisema: "Nahisi maisha yake yametolewa kafara kuifunza dunia kwamba ubakaji na aina kama hiyo ya tabia haiwezi kuendelea."
Wakati hukumu hiyo ilipotangazwa watuhumiwa wote walitawanyika mbali na Akshay Thakur.
Kila mmoja aliamriwa kulipa rupia 55,000 kwa familia ya mwathirika wao.
Katika risala yake ya kuhitimisha, Jaji Khanna alisema hangeweza kufumbia macho ongezeko la mashambulio ya udhalilishaji dhidi ya wanawake.
No comments:
Post a Comment