JE, WAJUA? KIATU CHAKO SASA CHAWEZA KUKUTAJIA UMRI ULIONAO...

Kuna njia nyingi za kuweza kutambua umri wako. Lakini wataalamu wamegundua njia ya ajabu ambayo hakika huwezi kuamini kwa urahisi. Sasa kiatu chako kinaweza kukupatia umri ulionao kwa sasa. Kivipi? Fuata maelekezo haya:

1. Andika namba unayovaa ya kiatu chako (Mfano: 6, 7 nk)
2. Namba hiyo zidisha kwa 5.
3. Jibu utakalopata jumlisha 50.
4. Jibu utakalopata zidisha kwa 20.
5. Jibu utakalopata jumlisha 1013.
6. Jibu utakalopata toa mwaka uliozaliwa (Mfano 1970, 1985 nk).
Kazi kwako...

No comments: