HUU NDIO UKWELI KUHUSU HALI YA SASA YA MZEE NELSON MANDELA...

Mzee Nelson Mandela.
Mzee Nelson Mandela bado yuko hospitalini akiwa mahututi lakini hali yake ikiendelea kuimarika, ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema jana.

Katika taarifa, ofisi ya Rais Jacob Zuma ilikanusha ripoti kwamba mpigania uhuru huyo wa zamani, ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, alikuwa ameruhusiwa kutoka hospitali hapo.
Taarifa za karibuni kuhusu hali shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi mwenye miaka 95 haijabadilika kutoka ilivyokuwa wiki iliyopita, wakati Zuma alisema Mandela alionyesha 'uthabiti mkubwa'.
"Madiba bado yuko hospitalini mjini Pretoria, na bado yuko mahututi lakini hali yake ikiimarika," ilisema taarifa hiyo, ikimtaja Mandela kwa jina lake la ukoo. "Taratibu hali yake imekuwa ikitetereka, lakini anaendelea vema na matibabu."
Mandela alilazwa kwenye hospitali hiyo ya Pretoria Juni 8 kwa kile maofisa walichosema ilikuwa kurejea kwa maambukizi kwenye mapafu.
Mandela ameendelea kuwa dhaifu mno, na taarifa chache zinazotolewa kuhusu hali yake zimekuwa zikidhibitiwa mno na familia yake na ofisi ya Zuma.
Zuma wiki iliyopita aliwataka wananchi wa Afrika Kusini kumwombea Mandela na kumweka kwenye fikra zao wakati wote.
Mahali pa makazi ya familia ya Mandela katika kitongoji tajiri kilichopo Johannesburg cha Houghton ni moja ya sehemu zilikofichwa siri mbaya za Afrika Kusini.
Mara kwa mara amekuwa akitembelewa na vyombo vya habari na wanaomtakia mema ambao huacha meseji mbalimbali za kumwombea apone haraka kwenye mawe yaliyopakwa rangi nje ya makazi hayo.
Mandela alitumikia miaka 27 kama mfungwa chini ya ubaguzi wa rangi na kisha akachomoza kujadiliana mwisho wa utawala wa weupe wachache kabla ya kuwa rais katika uchaguzi huru wa kwanza nchini humo mwaka 1994.
Alikuja kuwa kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini na rais wa kwanza mweusi mwaka 1994 baada ya shinikizo kutoka kote ulimwenguni, ikiwamo mgomo mkubwa, uliohitimisha vikosi vya ubaguzi wa rangi vya weupe wachache.

No comments: