Usain Bolt. |
Usain Bolt anapanga kustaafu mchezo wa riadha baada ya Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro mwaka 2016.
Bingwa huyo anayeshikilia rekodi ya sasa ya dunia kwenye mbio zote za mita 100 na 200, Mjamaica ana mkakati wa kuachana na mchezo huo ambao utamsimika kama mkongwe halisi wa michezo.
Bolt anaamini atashinda dhahabu mjini Rio, kuweka rekodi nyingine katika mita 200 mwaka ujao, na kunyakua medali ya dhahabu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow.
Na juu ya yote, atasherehekea siku yake ya mwisho ya kushiriki mchezo huo pamoja na kutimiza miaka umri wa miaka 30. Michezo hiyo ya Olimpiki 2016 mjini Rio imepangwa kuendelea hadi Agosti 21, siku ya sherehe ya kuzaliwa mwanaridha huyo.
Wakati akifichua mipango yake, Bolt alisema: "Nafikiri itakuwa muda muafaka kustaafu, juu na kuwa nimetamba kwa muda mrefu mno."
Baada ya kushinda medali nyingine tatu za dhahabu katika ubingwa wa dunia mjini Moscow, Bolt atakimbia mbio zake za mwisho msimu huu katika mita 100 Ijumaa kwenye Kumbukumbu ya Van Damme.
"Kama nataka kuwa miongoni mwa miamba (Muhammad) Ali na Pele na watu wote hawa natakiwa kuendelea kutawala hadi nitakapostaafu," aliongeza Bolt.
Akiwa na medali sita za dhahabu za Olimpiki na nane katika Ubingwa wa Dunia, hakuna hatari kubwa kwa bingwa huyo mwenye miaka 27 kuja kusahauliwa.
Bolt alinyakua medali tatu za dhahabu - kwenye mita 100, mita 200 na mita 4x100 - katika wiki za hivi karibuni mjini Moscow.
Kuondolewa mapema wakati wa fainali za mita 100 mjini Daegu miaka miwili iliyopita ni dosari pekee kwa mkimbiaji huyo mpaka sasa.
Wanariadha watatu tu - akiwamo Carl Lewis - ambao wana medali zaidi ya bingwa huyo wa sasa.
Endapo Bolt atatwaa medali tatu za dhahabu mjini Rio, atalingana na waliomtangulia katika rekodi ya mwanariadha bora kabisa kuwahi kutokea kwenye Michezo ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment