KUSHOTO: Princess Diana. KULIA: Gari walilopanda mara baada ya ajali hiyo. PICHA NDOGO: Dodi al Fayed. |
Polisi nchini Uingereza imesema juzi usiku ilikuwa ikikadiria kusadikika kwa taarifa mpya kuhusiana na vifo vya Princess Diana na Dodi Fayed ikiwamo madai kwamba waliuawa na askari wa jeshi la Uingereza.
Ilisema ilikuwa ikipima taarifa hizo, ambazo zimemhusisha Sajenti Danny Nightingale, mdunguzi wa SAS aliyetiwa hatiani kwa kuficha bastola na risasi 338 kinyume cha sheria ndani ya chumba chake.
Madai hayo yalijumuishwa kwenye barua kutoka kwa wakwe za Askari N, aliyekuwa zamani akiishi na Sajenti Nightingale, ambayo ilipelekwa kwa Ofisa wa kikosi cha SAS mnamo Septemba 2011.
Inafahamika taarifa hizo zilipitishwa kwa Makao Makuu ya Polisi kupitia Polisi wa Jeshi la Kifalme.
Barua hiyo inasema Askari N alidai SAS 'ina mkono kwenye kifo cha Princess Diana' na imekuwa 'ikikingiwa kifua', liliripoti gazeti la Sunday People.
Barua hiyo ilisema: ""Yeye (Askari N) pia alimweleza mkewe kwamba alikuwa XXX aliyepanga kifo cha Pricess Diana na kwamba amekuwa akikingiwa kifua."
Taarifa iliyotolewa na polisi wa Uingereza ilisema: " Polisi Makao Makuu inapitia taarifa ambazo ilizipokea hivi karibuni zenye uhusiano na vifo hivyo na kukadiria uhusiano na usadikikaji wake.
"Ukadiriaji huo utafanywa na maofisa kutoka wataalamu wa uhalifu na kikosi cha oparesheni.
"Huku sio kurudia uchunguzi na haijaja chini ya Operation Paget."
Polisi walisema hawajajiandaa kujadili suala hilo zaidi, huku msemaji wa malkia alisema hakutakuwa na maoni yoyote kuhusiana na suala hilo kutoka kwa Prince William, au Prince Harry, au kutoka Jumba la Clarence.
Diana na Dodi na dereva Henri Paul walifariki baada ya gari lao aina ya Mercedes kujibamiza kwenye barabara ya chini kwa chini, ambalo lilitoka kwenye Hoteli ya Ritz asubuhi ya Agosti 31, 1997.
Kesi ya vifo vya Diana na Dodi ilidumu kwa zaidi ya siku 90 huku ushahidi ukitolewa kutoka kwa takribani mashahidi 250.
Uchunguzi rasmi ulihitimishwa Aprili 7, 2008, huku mahakama ikitoa huku kwamba 'Princess wa Watu' na rafiki yake wa kiume waliuawa kinyume cha sheria.
Baada ya kesi, Polisi Makao Makuu ilisema imetumia Pauni za Uingereza milioni 8 kwa huduma zilizotokana na uchunguzi na uchunguzi wa Operation Paget kutoka 2004 hadi 2006.
Fedha hizo zinajumuisha gharama za wanasheria ambao walimwakilisha kamishna wa kikosi kwenye uchunguzi huo rasmi, ulinzi wa polisi kwa ajili la uchunguzi rasmi mahakamani na kulipia upelelezi wa Paget, iliripotiwa kuwa imegharimu Pauni milioni 3.6.
Uchunguzi wa Paget wa Kamishna wa zamani wa Polisi, Lord Stevens ulianza 2004 kwa maombi ya Michael Burgess, Ofisa Uchunguzi wa Vifo, ambaye wakati huo alikuwa akichunguza hatima ya upelelezi wa suala la Diana.
Polisi huyo wa zamani wa ngazi za juu alichapisha ripoti yake mnamo Desemba 2006, akitupilia mbali madai ya mauaji yaliyopigiwa kelele na baadhi ya watu, akiwamo baba wa Dodi, Mohamed al Fayed.
Uchunguzi wa Lord Stevens uligundua kwamba Diana hakuuawa na mashushushu wa Uingereza wala na Mtawala wa Edinburgh na kwamba hakuwa mjamzito wala kuvikwa pete ya uchumba na rafiki yake wa kiume, Dodi.
Operation Paget ilihitimisha, kama ilivyokuwa kwa uchunguzi wa Ufaransa mwaka 1999, kwamba dereva Henri Paul alikuwa amelewa na kuendesha kwa mwendo mkali mno.
Uchunguzi huo ulitupilia mbali njama mbalimbali zisizoisha zilizoibuliwa na ajali hiyo mbaya.
Paul alikuwa na kilevi cha takribani gramu 1.74 kwa lita mwilini wakati wa ajali hiyo - takribani mara mbili ya kiwango cha juu kabisa cha ulevi kwa dereva kinachoruhusiwa nchini Uingereza.
Mercedes S280 ya rangi nyeusi ilikuwa ikiendeshwa kupitia barabara ya chini kwa chini ya Pont de l'Alma mjini Paris kwa spidi ya takribani maili 61 hadi 63 kwa saa - mara mbili ya spidi ya mwisho inayoruhusiwa kwa kipande hicho cha barabara.
Lord Stevens alisema madai kwamba Diana aliuawa 'hakubainika' na kwamba hakubaini chochote kuhalalisha upelelezi zaidi na ndugu wa Familia hiyo ya Kifalme.
Msemaji wa al Fayed juzi alisema hana la kusema kuhusiana na taarifa hizo, lakini 'atapendelea kuona matokeo', akiongeza kwamba anaamini Polisi watachunguza taarifa hizo 'kwa bidii'.
Wizara ya Ulinzi ilisema jana haitoi maoni yoyote kuhusiana na suala hilo.

No comments:
Post a Comment