Thursday, August 8, 2013

SHEKHE PONDA AALIKWA KUONGOZA KONGAMANO LA BARAZA LA IDDI...

Shekhe Ponda Issa Ponda.
Wakati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ikimpiga marufuku Katibu wa Jumuiya ya Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda, kuendesha mihadhara ya kidini katika ardhi ya Zanzibar yenye mwelekeo wa kuleta mifarakano na uhasama kwa jamii, Umoja wa Wahadhiri wa dini ya Kiislamu Mkoa, umemwalika kuongoza kongamano la Baraza la Iddi.

Kongamano hilo limepangwa kufanyika siku ya Iddi Pili kwenye viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege mjini hapa.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kongamano hilo, Idd Msema, alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari kuwa Jeshi la Polisi limekubali kufanyika kwa kongamano hilo.
Kwa mujibu wa Msema, Polisi imetoa masharti kwamba yasitumike maneno ya kashfa dhidi ya dini zingine au kiongozi wa Serikali kwa kutumia vipaza sauti au sauti ya kawaida.
Barua ya Polisi ya kuruhusu kufanyika kongamano hilo, imenukuu kifungu namba 43 (1) na 44 ambacho kinalipa mamlaka Jeshi hilo kusimamisha mara moja mkutano kama huo mara itakapobainika kuwapo hali ya vurugu inayotishia amani na usalama.
Hata hivyo, alisema madhumuni ya kongamano hilo ni kukumbusha Waislamu masuala muhimu yahusuyo dini yao, hasa baada ya kutoka katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kwa mujibu wa Msema, kongamano hilo litashirikisha mashekhe wa wilaya zote za mkoa wa Morogoro, waumini wa dini ya Kiislamu na wasiokuwa waumini wa dini hiyo.
Pia alisema litajikita kujadili maisha baada ya Mfungo ambapo mashekhe pamoja na Ponda watatoa mhadhara huo.
Katibu wa Maandalizi ya Kongamano hilo, Nassoro Abdallah Nassoro, alisemaÊ wanatarajia Êumati mkubwa wa waumini na watu wengine watajitokeza Êkatika   kutokana na uwepo wa Shekhe Ponda.
Shekhe Ponda hivi karibuni alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya Mahakama kumkuta na hatia ya mashitaka aliyofunguliwa ya kuingilia kiwanja kilichoko Chang'ombe Markazi, kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza.

No comments: