Monday, July 8, 2013

WALIOKUFA AJALI YA NDEGE ILIYOANGUKA NA KUWAKA MOTO WATAMBULIWA...

PICHA KUBWA: Abiria wa ndege hiyo wakikimbia kutoka kwenye ndege hiyo mara baada ya kuanguka. PICHA NDOGO: Mabaki ya ndege hiyo baada ya kuteketea kwa moto.
Waathirika wawili ambao walikufa wakati ndege ya Asiana Airlines aina ya Boeing 777 ilipoanguka na kuwaka moto wakati ikitua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa San Francisco juzi  asubuhi wametambuliwa kuwa ni wanafunzi wa kike kutoka China ambao walikuwa kwenye safari ya kimasomo.

Miili hiyo ya Ye Mengyuan na Wang Linjia, wote wenye umri wa miaka 16, ilikutwa kwenye njia ya kuruka/kutua baada ya mkia wa ndege hiyo, ambayo ilikuwa ikitokea mjini Seoul, Korea ya Kusini ikiwa na watu 307 ndani yake, kunyofoka huku ndege hiyo ikijibamiza kwenye eneo la uelekeo wa njia ya kuruka/kutua wakati ikija kutua muda mfupi kabla ya Saa 5:30 asubuhi.
Wasichana hao, ambao walitambuliwa na shirika la habari la China jana, walikuwa sehemu ya kundi la wanafunzi 29 na walimu watano ambao walitokea Shule ya Kati ya Jiangshan - shule yenye ushindani mkubwa mjini Zhejiang huko mashariki mwa China. Wote walikuwa wameketi karibu na nyuma ya ndege.
Kwa namna ya kushangaza, watu 305 waliosalia kwenye ndege hiyo walinusurika lakini zaidi ya watu 180 walijeruhiwa baada ya ndege hiyo kugeuka kimondo.
Picha za kutisha zilizopigwa na walionusurika muda mfupi baada ya kuanguka zilionesha abiria wakichomoza kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo na kuharakisha kuondoka kwenye eneo hilo. Moshi mzito kisha ukafuka kutoka kwenye kiunzi cha ndege, na picha za televisheni baadaye zilionesha ndege hiyo ikiacha nyeusi kutokana na moto, huku sehemu kubwa ya paa lake ikiwa imeteketea kabisa.
Wakati wengi wa abiria hao wakifanikiwa kutoka kwenye ndege hiyo kwa kutumia milango ya dharura ya kuserereka, baadhi ya walionusurika pia walionekana kwenye maji kando tu ya njia hiyo ya kuruka/kutua.
"Baadhi ya abiria walishuhudiwa wakitokea kwenye maji - kwa hisia kwamba walijitosa wenyewe," alisema Joanne Hayes-White, mkuu wa kikosi cha zimamoto San Francisco.
Hospitali za mjini humo ziliwatibu abiria 182 huku watu wazima wapatao watatu na watoto wawili wanasemekana hali zao ni mbaya. Takribani 49 wako mahututi wakati abiria 123 walipata majeraha madogo katika ajali hiyo.
Hakuna dalili zozote za haraka za chanzo cha ajali hiyo na wachunguzi wa Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafirishaji walikuwa wakitarajiwa kufika kwenye uwanja huo wa ndege majira ya usiku wa manane kuanza uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.
Asiana Airlines ilisema haioneshi kwamba ajali hiyo imesababishwa na hitilafu za kiufundi ingawa imekanusha shutuma za pengine rubani huyo au makosa kwenye mnara wa kuongozea ndege.
Katika kioja cha kuchanganya, abiria Lee Jang Hyung alieleza juzi usiku kwamba baada ya ndege hiyo kusimama kufuatia migongano kadhaa, sauti ilisikika kupitia mawasiliano ya ndani ikiwataarifu abiria hao waliojawa hofu kwamba Ndege 214 imetua salama na kila mmoja atulie kwenye kiti chake.
Kwa mujibu wa Asiana Airlines, abiria 141 kati ya wote waliokuwamo ndani ya Ndege 214 ni Wachina, Wakorea Kusini 77 , Wamarekani 61, na mmoja ni Mjapani.
"Tunaungana na kuwaombea abiria wote. Tumesikitishwa mno na tukio hili," alisema Meya wa San Francisco, Edwin Lee wakati akitoa taarifa za tukio hilo.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari baadaye jioni hiyo, Meya Lee alisema: "Ni miujiza na bahati kubwa kwamba tunao walionusurika wengi."
Wafanyakazi 16 walikuwamo ndani ya ndege hiyo.
 

MATUKIO MATANO MABAYA ZAIDI YA KUANGUKA NDEGE NCHINI MAREKANI TANGU 2001:

Februari 12, 2009: Cologan Air Dash Q-400; karibu na Buffalo, NY: Ndege hiyo ilianguka kwenye eneo la makazi na kuua abiria 44 na wafanyakazi wanne, sambamba na mtu mmoja aliyekuwa chini.
Agosti 27, 2006: Comair CRJ-100; Lexington, KY:
Ndege hiyo ilikuwa ya safari za ndani ya nchi kutoka Lexington, KY kwenda Atlanta, GA. Ndege hiyo ilianguka baada ya kuruka na kuua wafanyakazi wawili kati ya watatu na abiria wote 47.
Desemba 19, 2005: Chalk ya Ocean Airways Grumman G-73T Mallard; Miami, FL: Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka Miami kuelekea kisiwa cha Bimini ilipata hitilafu za kiufundi. Ndege hiyo ilianguka Biscayne Bay, na kuua abiria wote 18 na wafanyakazi wote waliokuwamo ndani yake.
Januari 8, 2003:Express Beech ya US Airways 1900; Charlotte, NC: Ndege hiyo ilianguka kwenye jengo la karakana kwenye uwanja wa ndege, na kuua marubani wote na abiria wote 19.
Novemba 12, 2001: American Airlines A300; Queens, New York: Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka New York kwenda Santa Domingo, Jamhuri ya Dominika ndipo ikaanguka kwenye eneo jirani la makazi nje kidogo ya Uwanja wa Ndege wa JFK, na kuua watu watano waliokuwa chini, abiria wote 251 wakiwamo watoto wachanga watano na wafanyakazi wote tisa.

No comments: