Thursday, July 4, 2013

SAINI YA PAPA FRANCIS YASUBIRIWA ILI KUMTANGAZA JOHN PAUL MTAKATIFU...

Papa John Paul II.
Papa John Paul II amevuka kigingi cha mwisho kabla ya kutajwa kuwa mtakatifu, akisubiria tu uthibitisho wa mwisho kutoka kwa Papa Francis I na siku ya sherehe ambayo itakuja mapema kabla ya Desemba 8, ofisa mmoja wa Vatican na ripoti za vyombo vya habari zilisema Jumanne.

Shirika la habari la ANSA liliripoti kwamba tume ya makardinali na maaskofu lilikutana Jumanne kujadili suala hilo la John Paul na kusaini kukubaliana nalo.
Ofisa mmoja wa Vatican alithibitisha kwamba uamuzi huo umechukua muda mrefu kiasi na kwamba mkutano wa Jumanne ulikuwa muhimu wa kukamilisha taratibu.
Moja ya siku zinazotarajiwa kuthibitishwa rasmi ni Desemba 8, karamu ya Dhana ya Imakulata, karamu kuu kwa Kanisa Katoliki. Mwaka huu karamu hiyo kwa bahati imeangukia siku ya Jumapili, siku ambayo kwa kawaida uthibitishwaji hufanyika.
Ofisa huyo, ambaye aliongea kwa sharti la kutotajwa jina sababu hajaidhinishwa na kanisa kujadili masuala ya utangazaji watakatifu kwenye kumbukumbu, alithibitisha ripoti hizo katika gazeti la La Stampa kwamba Papa John Paul II atathibitishwa pamoja na Papa John XXIII, ambaye aliitisha Baraza hilo la Pili la Vatican lakini akafariki mwaka 1963 kabla halijamaliza muda wake.
Kuna sababu kadhaa kwa uthibitishwaji mapapa wawili pamoja, kubwa kulinganisha mmoja baada ya mwingine.
John Paul II amekuwa mstari wa mbele katika uwezekano wa utakatifu tangu kifo chake mwaka 2005, lakini kumebaki hoja kadhaa kwamba mchakato huo umekuwa wa haraka mno.
Wakati wa misa ya mazishi ya Papa John Paul II mwaka 2005, kelele za 'Santo Subito!' au 'Utakatifu Sasa!' zililipuka kwenye Kanisa Kuu la Mt. Petro.

No comments: