Thursday, July 4, 2013

NDEGE ZABADILI UELEKEO BAADA YA ABIRIA KULAZIMISHA AFUNGUE MLANGO ANGANI AKAVUTE SIGARA...

Mojawapo ya Ndege hizo ikiwa angani.
Mwanaume mmoja wa New York amesababisha ndege mbili kubadili uelekeo katika kipindi kisichozidi masaa mawili baada ya kuwa amejaribu kufungua mlango wa ndege kuweza kwenda kuvuta sigara wakati ndege hiyo ikiwa angani.

Katika matukio yote mawili mwanaume huyo alijaribu kuwasha sigara ndani ya ndege hiyo kabla ya kuelekea kwenye mlango wa kutokea, na kulazimisha ndege hiyo kubadili uelekeo.
Vurugu za kwanza zilitokea katika ndege ya usiku kutoka Las Vegas kwenda Charlotte, North Carolina, ambayo ililazimika kutua mjini Albuquerque.
Mwanaume huyo, ambaye aliripotiwa kuongea kwa lafudhi ya Kirusi, alikuwa akitikisa kiti cha mbele yake, akijaribu kuwasha sigara na kwenda kwenye mlango 'kutoka kwa ajili ya kuvuta sigara,' mamlaka zilieleza.
Mwanaume huyo alihojiwa na polisi na FBI lakini kwa kuwa alikuwa hakufanikiwa kufungua mlango huo, aliachiwa huru bila kufunguliwa mashitaka.
Kufuatia kuachiwa kwake, mwanaume huyo alikata tiketi ya ndege inayoelekea Chicago kwenye shirika jingine ambako alirudia tabia yake hiyo.
Abiria waliripoti kwamba mwanaume huyo kwa mara nyingine tena alijaribu kuwasha sigara ndani ya ndege hiyo na kugoma kukaa kwenye kiti.
Akiwa kwenye ndege hiyo kuelekea Charlotte, alijaribu kufungua mlango wa ndege.
Ofisa mmoja wa FBI aliyekuwa mapumzikoni na abiria kadhaa walimdhibiti mwanaume huyo na ndege hiyo ikalazimisha kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kansas City majira ya Saa 5:30 asubuhi.
Kwa mujibu wa abiria mwingine mwanaume huyo alizungumza Kirusi na 'kuendelea kujaribu kufungua mlango wa kutokea kwenda nje na ili akavute sigara.
Mwanaume huyo alisindikizwa kutolewa nje na ndege hiyo ikaweza kuendelea kwenda Chicago saa moja baadaye.
Kwa mara nyingine tena alihojiwa na mamlaka husika na kuachiwa huru bila ya kushitakiwa mjini Kansas City.

No comments: