Friday, July 5, 2013

CHEKA TARATIBU...

Wavuta dawa za kulevya wawili 'maarufu kama mateja' walikuwa wakihangaika kutungua maembe kwenye mti bila mafanikio.
Baada ya takribani saa nzima teja mmoja akamwambia mwenzake: "Oyaa, wacha nipande juu ya mti nikacheki kama zimeiva." Kweli yule teja akapanda hadi juu na kutomasa yake maembe na kuyaacha kisha akashuka chini na kumwambia mwenzake: "Yameiva fresh msela wangu! Sasa ongeza mawe tuendelee na kazi!" Kasheshe...

No comments: