SHUKRANI
CASSIUS MGAVINYI
BERNARD KIBASSA
05 JULAI 1963 – 12
APRILI 2013
Ilikuwa usiku wa tarehe 12 Aprili 2013 tulipopigiwa simu na
kupewa taarifa kuwa mpendwa wetu Cassius hayuko nasi tena.
Cassius tunajua kuwa kila kizaliwacho hakina budi kufa,
lakini tunakiri kuwa tulipata mstuko mkubwa ambao mpaka sasa bado tunaona kama
ndoto. Hata hivyo tukiwa na imani
inatubidi kukubali kuwa kila mwana adamu amepangiwa kifo chake, Mapenzi ya
Bwana Yatimizwe.
Kwa namna ya pekee tunapenda kutoa shukrani kwa Uongozi na
Ofisi ya Bunge Dodoma na Dar es Salaam kwa misaada yote na kwa kushirikiana
nasi katikam kipindi hiki kigumu katika matayarisho na hatimaye kumpumzisha
katika nyumba ya milele mpendwa wetu Cassius.
Kwa kuwa si rahisi kumshukuru
kila mtu, basi familia ingependa kutoa shukrani za pekee kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano, Mhe. Anna Makinda, Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai, Katibu wa Bunge,
Mhe. Dkt Thomas Kashililah, Mhe. William Lukuvi (Mb), Mhe. Steven Wassira (Mb),
Mhe. Margareth Sitta (Mb), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Mama Kipa,
Mhe. Profesa Msola (Mb) na Mkuu wa Mkoa Iringa, Mama Christine Ishengoma.
Vile vile tunapenda kuwashukuru sana ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote wa Dodoma na Dar es Salaam
ambao walikuwa bega kwa bega nasi, Baba na Mama Mtenga wa Kikuyu, Jumuiya ya
Mtakatifu Matilda ya Dodoma, Baba Paroko
wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Dodoma, bila kuwasahau ndugu, jamaa na
marafiki wote wa Iringa mjini na kijijini Nyabula kwa namna ambavyo tumekuwa pamoja
mpaka kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu Cassius.
Mkesha wa kumaliza msiba utafanyika kijijini Nyabula, Iringa
mnamo tarehe 13 Juni 2013 na tarehe 14 Juni 2013 kutakuwa na Misa ya kumuombea mpendwa
wetu itakayofuatiwa na kusimika msalaba itakayofanyikia kijijini Malendi,
Iringa. Baada ya hapo tunaomba wote
tujumuike kwa chakula cha mchana hapo Malendi, Nyabula.
RAHA YA MILELE UMPE E
BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI, AMINA.

No comments:
Post a Comment