Tuesday, May 14, 2013

NDEGE YATUA KWA DHARURA BAADA YA MWANAMKE KUGOMA KUACHA KUIMBA...

Askari wakimdhibiti mwanamke huyo ndani ya ndege.
Rubani wa American Airlines alilazimika kutua kwa dharura ndege hiyo baada ya abiria mmoja kugoma kuacha kuimba wimbo uliotamba wa Whitney Houston wa 'I Will Always Love You'.

Mtumbuizaji huyo wa kujitegemea alianza muda mfupi katika safari ya ndege kutoka Los Angeles kwenda New York na kuimba kwake kwa sauti ndogo kukaongezeka mno na kuwa kero kwa abiria na wafanyakazi wa ndege hiyo inayofanya safari za ndani Alhamisi iliyopita.
Rubani huyo alilazimika kubadili uelekeo wa ndege hiyo nusu ya safari hiyo ya saa sita na kufanya kituo cha ghafla kwenye uwanja wa ndege wa Kansas City hivyo kuwezesha maofisa kumtoa mwanamke huyo kutoka kwenye ndege hiyo.
Msemaji wa uwanja wa ndege, Joe McBride alisema: "Mwanamke huyo alikuwa msumbufu na aliondoshwa kutoka kwenye ndege hiyo kwa kuzozana na wafanyakazi wa ndege hiyo.
"Kulikuwa na askari mmoja ndani ya ndege hiyo, ambaye alimkabili mwanamke huyo na kumfunga pingu na kumshusha kwenye ndege hiyo."
Licha ya wafanyakazi kuwaeleza abiria hawaruhusiwi kupiga picha wakati wakiwa ndani ya ndege, mmoja alifanikiwa kurekodi video fupi ya mwanamke huyo akisindikizwa kushuka kwenye ndege hiyo akiwa amefungwa pingu - huku bado akiwa anaimba wimbo huo wa pop wa miaka ya 1990.
Wakati wimbo aliochagua kuwatumbuiza abiria wenzake unafahamika mno katika filamu ya Whitney Houston ya Bodyguard, asili yake uliimbwa na mwimbaji wa miondoko ya country, Dolly Parton mwaka 1974.
Wimbo halisi wa 'I Will Always Love You' ulipokelewa vizuri na wadau na kufanikiwa kushika namba moja katika chati za Billboard kwa nyimbo kali za Hot Country mara mbili.
Hii ilimfanya Parton kuwa msanii wa kwanza katika historia kushika rekodi namba moja mara mbili kwa wimbo mmoja kama mwimbaji , na mara tatu kama mwandishi.
Lakini haikuwa hadi Whitney aliporudia I Will Always Love You katika filamu ya Bodyguard ndipo wimbo huo ukaja kushika chati kimataifa.

No comments: