Saturday, May 18, 2013

MTAALAMU WA TIBA YA UREMBO AFA KWA KUNYWA SUMU AKIDHANI POMBE...

Cheznye Emmons enzi za uhai wake.
Mtaalamu wa tiba ya urembo wa Uingereza amefariki dunia baada ya kunywa pombe iliyowekwa sumu wakati akifanya safari ndefu katika msitu mnene nchini Indonesia.

Cheznye Emmons, kutoka Great Wakering, Essex, alianza kuumwa baada ya kunywa kimiminika hicho kutoka kwenye chupa iliyowekwa lebo ya 'gin' (aina ya pombe kali) ambayo baadaye ilibadilishwa na kujazwa sumu hatari ya Methanol.
Mwanamke huyo mwenye miaka 23 alikuwa akisafiri kuzunguka kusini mwa Asia akiwa na mpenzi wake Joe Cook, mwenye miaka 21, na rafiki wa kiume wa wapenzi hao alikutana nao katika safari yao ndipo wakanunua pombe hiyo iliyotia doa kutoka kwenye duka moja nchini Indonesia.
Methanol in a sumu kali na inafahamika kwa kusababisha figo kushindwa kufanya kazi, upofu, mshituko wa moyo na kifo - huku kiasi kidogo cha hadi mililita 30 kinaweza kuhatarisha maisha ya mtu mzima.
Kodi kubwa zimesababisha kupanda mno kwa bei ya mvinyo uliozalizwa, bia na pombe kali katika nchi hiyo ya Kiislamu na hivyo kuhamamisha matumizi ya pombe kali zinazoandaliwa kienyeji maarufu kama 'arak' - lakini baadhi ya  wasambazaji wasiokuwa waaminifu wamefika mbali zaidi, wakiongezea Methanol hatari kwenye pombe kali za kienyeji.
Kifo hicho cha Cheznye sio kesi pekee - mnamo 2009, watu 25 - wakiwamo Waingereza wawili walifariki baada ya kunywa pombe hiyo ya 'arak' iliyochanganywa na Methanol nchini Bali.
Wasafiri wote hao watatu walianza kuumwa ndani ya masaa kadhaa kutokana na kutumia kitu chenye sumu wakati wakiwa wamepiga kambi kwenye msitu huo mnene.
Lakini ndani ya siku kadhaa mtaalamu huyo hali yake ikabadilika na kuwa mbaya na kulalamika kuwa hawezi kumwona mpenzi wake.
Walienda kutafuta msaada wa matibabu, lakini iliwachukua masaa kadhaa ya kusafiri katikati ya msitu huo mnene kabla ya kufikia kliniki ya macho.
Walipowasili Cheznye haraka akahamishiwa kwenye hospitali moja iliyoko Medan, Sumatra, ambako aliwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Mnamo Aprili 25, wazazi wa Cheznye Pamela na Brenton walichukua uamuzi wa kushitusha kuzima mashine yake ya kupumulia baada ya kuwa wamesafiri kwa ndege hospitalini hapo kumuuguza binti yao.
Cheznye au Chez kama anavyoitwa na mpenzi wake, ni wa mwisho kati ya ndugu zake wanne.
Ana dada zake wawili, Bianca mwenye miaka 34, na Measha mwenye miaka 26 na kaka Michael mwenye miaka 33.
Akiwa na huzuni tele Michael alisema: "Siamini kama ni kweli. Tumepatwa na mshituko.
"Kwa tunavyoelewa, duka hilo litakuwa lilimwaga 'gin' hiyo kutoka chupa yake halisi na kisha kujaza methanol.
"Ilikuwa kwenye chupa halisi pamoja na lebo yake ya 'gin'.
"Kwa sasa tunafahamu, duka lililouza pombe hiyo limefungwa na kwamba kuna uchunguzi wa polisi unaendelea. Ubalozi wa Uingereza pia unafuatilia hili kwa ukaribu.
"Tunaamini hili halijafagiliwa chini ya zulia kama ambavyo baadhi ya vitu hivi vinavyofanyika."
Idadi ya watalii wanaokufa kutokana na sumu kwenye pombe nchini Indonesia inaongezeka.
Juni mwaka jana raia wa Swedenm, Johan Lundin, mwenye miaka 28, aliwekewa sumu katika pombe ya mojito iliyochanganywa na methanol baada ya kunywa kwenye baa moja iliyoko kisiwa cha Gili Trawangan karibu na Bali.
Mchumba wake, Michaela Pechac, alishuhudia kwa hofu wakati Johan akifariki dunia.

No comments: