![]() |
| Rais Jakaya Kikwete. |
Matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka jana, yameigusa Serikali ambayo imesema itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hali hiyo haijirudii.
Hayo yamo katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ambayo aliitoa juzi kwa Taifa katika utaratibu aliojiwekea wa kuhutubia Taifa kila mwisho wa mwezi.
“Napenda kuwahakikishia kuwa sisi katika Serikali tumetoa kipaumbele cha juu sana kwa elimu na kwamba hakuna upungufu wa utashi kwa upande wangu na wenzangu wote Serikalini. Ndiyo maana tumeguswa sana na matokeo haya,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa Serikali yake inaipa kipaumbele sekta ya elimu nchini na ndiyo sababu ina bajeti kubwa kuliko zote ambayo ni Sh trilioni 3.6 sawa na asilimia 24 ya bajeti ya Serikali.
Alisema pamoja na matatizo hayo kujitokeza, bado “tutaendelea kutoa kipaumbele cha juu kwa elimu mpaka hapo itakapofikia mahali matatizo makubwa yatakapokuwa yamepungua sana.”
Rais alitoa ufafanuzi wa yaliyojitokeza katika mitihani hiyo, uzito wa tatizo na kuelezea sababu zilizomsukuma Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya kujua kiini cha asilimia 60 ya watahiniwa hao kufeli mitihani hiyo.
Alizungumzia kiwango cha ufaulu kushuka ghafla, kutoka asilimia 53.6 mwaka 2011 hadi asilimia 34.5 mwaka 2012 akisema ni anguko la asilimia 19.1 ambalo, ni kubwa sana.
Lakini pia alisema hata shule zinazofahamika kuwa na historia ya kufaulisha vizuri kama seminari, shule za binafsi, za mashirika ya dini na sekondari kongwe za Serikali ambazo hazina matatizo kama ilivyo kwa sekondari za kata, nazo safari hii hazikupata mafanikio kama ilivyo kawaida yao.
“Nazo zimejikuta zikiwa na idadi ya vijana waliopata daraja la kwanza, la pili na la tatu ikipungua wakati waliopata daraja la nne na waliofeli wakiongezeka. Isitoshe na kiwango cha ufaulu wa vijana kimepungua pia.
“Mwaka 2010 wanafunzi 10 bora wote walikuwa wamefaulu daraja la kwanza la alama au pointi saba. Mwaka 2011 katika wanafunzi 10 bora, wanane walipata daraja la kwanza kwa alama saba na wawili alama nane. Mwaka 2012 katika wanafunzi 10 bora, watatu walipata daraja la kwanza kwa alama tisa, watatu alama 10 na wawili alama 11,” alisema Rais.
Alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo, ndiyo sababu kila mtu amekuwa na mawazo yake yakiwamo ya kusukumia walimu, wanafunzi na hata Serikali yenyewe, na hivyo Tume itakayoundwa ndiyo itakuja na majibu sahihi na aliwataka wananchi kushiriki kutoa mawazo yao.
“Sisi katika Serikali hatuwezi kuwa tunadhani, kwa sababu tunayo dhamana maalumu. Lazima tujue ukweli kwa uhakika na ndiyo maana kuna umuhimu wa Tume,” alisema.
Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) wanafunzi 397,132 walifanya mtihani huo na kati yao, waliofaulu ni 126,851 sawa na asilimia 34.5. Wanafunzi 240,903 sawa na asilimia 65.5 hawakufaulu.
Mwaka 2011, wanafunzi 336,782 walifanya mtihani huo na waliofaulu walikuwa asilimia 53.6 na ambao hawakufaulu kabisa walikuwa asilimia 46.4. Mwaka 2010 wanafunzi 352,045 walifanya mtihani asilimia 50.4 walifaulu na asilimia 49.6 hawakufaulu.
Akizungumzia uhusiano wa Waislamu na Wakristo, alisema kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka jana, kumekuwa na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini hizo akiyataja kuwa ni kauli na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini hizo, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje.
Alisema kauli hizo zimekuwa zikipitia vyombo vya habari, mitandao ya kompyuta na hata simu za mikononi na kusababisha mitafaruku hata upotevu wa maisha, akitolea mifano ya Buseresere, Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar.
“Kuna wenzetu kwa sababu wanazozijua wao na kwa manufaa wanayoyajua wao, wanataka kutuvurugia nchi yetu hii nzuri. Tusiwape nafasi wachochezi hawa, kwani hawatutakii mema na wala hawazitakii mema dini zetu na nchi yetu.
“Sisi katika Serikali, hatutasita kuwachukulia hatua wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine. Nimewakumbusha polisi na mamlaka husika kote nchini, wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika,” alifafanua Rais.
Aliongeza kuwa amelitaka Jeshi la Polisi nchini kukamilisha mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini nchini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

No comments:
Post a Comment