Imani ya wagombea wa urais wanaoongoza katika uchaguzi mkuu nchini, imeanza kupungua baada ya Muungano wa Cord, unaoongozwa na Raila Odinga, kudai kubaini rafu katika matokeo yanayoendelea kutangazwa.
Mgombea Mwenza wa Odinga, Kalonzo Musyoka jana aliwaambia waandishi wa habari kwamba matokeo waliyopewa yameonesha kuwa na utata.
“Tuna ushahidi kwamba matokeo tuliyopewa yana utata,” alidai Musyoka, huku akiongeza kuwa katika baadhi ya matokeo waliyopewa, yanazidi idadi ya wapiga kura halisi waliojiandikisha.
Kutokana na utata huo, Musyoka ametaka utaratibu wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo usitishwe, kutokana na matokeo kuwa na utata.
Hata hivyo, jana jioni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Isaack Hassan, alisema hawajapata matokeo yaliyoonesha kuzidi wapiga kura waliojiandikisha.
Hassan alitaka Wakenya kuacha kusikiliza maneno hayo ya wanasiasa, yakiwamo ya kubashiri mshindi, kwa kuwa hata yeye hajui matokeo yatakuwaje, kwa sababu bado wanaendelea kuhesabu na kupokea matokeo.
Alisema wajumbe wa Tume walikula kiapo na hakuna ambaye amepiga kura na wamejizatiti kuhakikisha hakuna uchakachuaji.
Alitoa mfano wa matokeo yaliyotangazwa katika majimbo, kwamba ni halisi yanayoelezea viongozi halisi waliochaguliwa na Wakenya.
Juzi Muungano wa Jubilee unaoongozwa na Uhuru Kenyatta, ulidai kuwa IEBC, unashinikizwa kuhesabu kura zilizoharibika na halali ili kuunyima ushindi muungano huo.
Hofu ya muungano wa Jubilee katika madai hayo yaliyowasilishwa kwa waandishi wa habari na Mgombea Mwenza wa Kenyatta, William Ruto, na upo uwezekano wa wagombea hao kulazimishwa kurudia uchaguzi katika raundi ya pili.
Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, ili mtu atangazwe mshindi katika urais, ni lazima apate ushindi wa zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa na angalau asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo 24. Kenya ina majimbo 47.
Kutokana na kura zilizoharibika kuongezeka na kuzidi 334,080, kama zikijumuishwa kupata idadi kamili ya kura na kila mgombea kutoa kura halali alizopata, kuna uwezekano wa kurudia raundi ya pili kwa wawili hao, kutokana na uwezekano wa kila mmoja kutozidi asilimia ya kura zilizopigwa kama inavyotakiwa na Katiba.
Hata hivyo, Musyoka katika tamko lake, alionya kuwa tuhuma zake hazimaanishi wananchi wachukue sheria mkononi kwa kuwa chama chake kinafuata utaratibu, kanuni na sheria zilizopo.
Kanisa Katoliki nchini, limeomba wananchi kuipa muda Tume ikamilishe kuhesabu kura na kutoa matokeo ya urais kwa wakati.
Muungano wa Jubilee nao jana ulitoa taarifa ukihoji mwenendo wa utaratibu wa kura kuhesabiwa, huku mmoja wa maofisa akiongeza kuwa kura nyingi zilizoharibika zinaleta utata na huenda zimeharibiwa makusudi.
Kutokana na tuhuma hizo, IEBC ilifanya mkutano wa ndani ukihusisha baadhi ya makamishna na mabalozi na Mwenyekiti wa Tume anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu tuhuma hizo leo.
Hadi jana jioni, Kenyatta alikuwa akiongoza kwa kura za urais milioni 2.7 akifuatiwa na Odinga aliyepata kura milioni 2, Musalia Mudavadi akipata kura 154,708, Peter Kenneth 25,008, Martha Karua 16,383, James ole Kiyiapi 15,500, Mohammed Dida 14,106 na Paul Muite kura 4,842. Matokeo kamili yanatazamiwa leo au Jumatatu.

No comments:
Post a Comment