![]() |
| Kardinali Peter Turkson. |
Kardinali Peter Turkson wa Ghana hawanii upapa, lakini ni dhahiri ana wanaomwunga mkono ambao wanaamini anatosha na wamebandika mabango yenye picha yake sehemu mbalimbali za jiji hili.
“Chagua Peter Kodwo Appiah Turkson kwenye Baraza la Makadinali!,” imeandikwa kwa herufi nzito katika mabango juu ya picha ya Kadinali huyo, ambaye ni maarufu miongoni mwa makadinali wanaofikiriwa kumrithi Benedict, ambaye Alhamisi alikuwa papa wa kwanza baada ya karne sita, kujiuzulu.
Mabango hayo yamebandikwa katika mbao ambazo zilitumiwa na wagombea wa uongozi nchini mapema wiki hii.
Tofauti na uchaguzi wa Bunge, wagombea wa upapa kwa kawaida hawatakiwi kuzindua kampeni, hali inayoonesha kuwa mabango hayo yanatoka kwa wafuasi wa Turkson au yawezekana yanabandikwa na wafanya mzaha.
Makadinali wanatarajia kukutana faragha katika kanisa dogo la Sistine kwa siku 10, mkutano ambao chaguo lao litakuwa limebarikiwa na Roho Mtakatifu na si siasa za kidunia.
Turkson anaweza kuwa mtu wa kwanza asiyetoka Ulaya kuongoza Kanisa Katoliki baada ya kipindi cha zaidi ya miaka 1,000 kupita kama atachaguliwa.
Lakini usemi wa zamani wa Kiroma unaonya dhidi ya kukampeni, hata kama ni kwa siri, ili mtu kuwa papa au hata kujaribu kubashiri matokeo ya Baraza la Makadinali. Unasema: “Anayeingia kwenye Baraza kama papa, anatoka kama kadinali”.
Wakati hayo yakiendelea, Papa mstaafu alikuwa akiendelea kusoma ujumbe kutoka kwa wanaomtakia heri huku akivinjari katika bustani za kasri lake.
Papa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 85 alikuwa pia akiangalia televisheni ikirusha matangazo ya kuondoka kwake Vatican Alhamisi jioni, na kulala fofofo katika makazi yake hayo ya upapa katika kasri la Gandolfo, ambako atakaa kwa miezi miwili, msemaji wa Vatican alisema jana.
“Alilala vizuri. Hali ya hewa ilikuwa mwanana yenye utulivu,” Padri Federico Lombardi aliwaambia waandishi wa habari, akikariri alichoambiwa na Katibu Myeka wa papa mstaafu, Askofu Mkuu Georg Gaenswein kupitia simu kutoka makazi hayo yaliyoko Kusini mwa Roma.
Benedict alichukua CD zake za muziki anaoupenda sana na vitabu vingi vya Theolojia, Historia na Falsafa, Lombardi alisema na kuongeza kuwa hivi karibuni ataanza kupiga kinanda chake usiku.
Kuhusu lini Baraza la kumchagua Papa mpya litaanza, makadinali ndio watakaoamua, lakini hilo halitafanyika mpaka idadi ya makadinali 115 kutoka sehemu mbalimbali duniani watakapokuwa wamewasili.
Haijulikani ni wangapi mpaka jana walikuwa wamewasili. Hakuna kilichokuwa kimeshaandaliwa hadi jana, lakini Vatican inaonekana kujipanga kwa uchaguzi ifikapo katikati ya mwezi huu, hivyo Papa mpya anaweza kusimikwa kabla ya Jumapili ya Matawi Machi 24 na hivyo kuongoza Wiki Takatifu kujiandaa na Pasaka Jumapili ifuatayo.
“Kila mtu, akiwamo yeye, anataka mkutano huo ufanyike haraka,” Kardinali wa New York, Timothy Dolan aliiambia Reuters. “Hatuna Papa na tunataka tuwe naye.
Sote hapa huko nyumbani tuna kazi za kufanya, hivyo tunataka kurejea makwetu.” Mbali na Turkson ambaye anapewa nafasi na kupigiwa upatu, wengine ni Leonardo Sandri wa Argentina, Christoph Schoenborn wa Austria, Odilo Scherer wa Brazil, Marc Ouellet wa Canada na Angelo Scola wa Italia.
Makadinali watatu kutoka Marekani waliwaambia waandishi wa habari Alhamisi jioni njia nyingi za kupima wagombea kama hakuna majina yatakayotangazwa
“Mjadala tulionao katika mabaraza kama haya utahusu zaidi maandalizi ya kiakili,” kwa ajili ya kuchagua Papa, alisema uchaguzi huo, lakini pia kwa maombi ya kina. Alisema amekuwa akitumia “intaneti sana” kuwasoma, kuwajua na kuwaelewa makadinali wengine.
Kadinali Francis George wa Chicago, alisema makadinali tayari wana taarifa nyingi na wamewataka wapiga kura wengine kupata taarifa zaidi, akihoji “unajua nini kuhusu mgombea huyu?” au “ni mtu wa aina gani?”
"Hebu fikiria kila mmoja wetu ana orodha mbili; ya wagombea wa chini na wa juu,” alisema na kuongeza kuwa orodha hiyo ya kidhahania inaweza kubadilika kadri mikutano hii ya awali kabla ya Baraza inavyoendelea.
Kadinali Daniel DiNardo wa Galveston-Houston, alisema alikuwa akisoma juu ya makadinali wengine na kwa kina zaidi juu ya upapa wenyewe na umuhimu wake kwa Kanisa.
Makadinali hawataona ripoti ya siri kubwa iliyoandaliwa kuhusu Papa Benedict kuhusu utawala mbovu na mgogoro ndani ya Curia-urasimu wa Kanisa.
Lakini waandaaji wa taarifa hiyo ambao ni makadinali watatu wataingia katika Baraza la Uchaguzi kuwashauri wapiga kura kuhusiana na ripoti hiyo.
"Kwa kuwa hatujui kilicho kwenye ripoti, nadhani tutategemea makadinali hao katika Baraza kutuelewesha kile wanachodhani kitakuwa na manufaa kwetu, kujua na kufanya uamuzi wa haki kwa ajili ya mustakabali wa Kanisa,” alisema O’Malley.

No comments:
Post a Comment