KARDINALI WA GHANA ATAJWA KUMRITHI PAPA BENEDICT XVI...

Papa Benedict XVI mara baada ya kutangaza kuachia ngazi ya uongozi katika Kanisa Katoliki. KULIA: Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson wa Ghana anayetajwa kuchukua mikoba hiyo.
Ndani ya dakika kadhaa tangu tangazo la kujiuzulu kwa Papa Benedict, minong'ono iliibuka kwa kasi kuhusu nani atakayemrithi Baba huyo Mtakatifu.
Kuna mapapa kadhaa wanaowania nafasi hiyo, lakini hakuna anayejihakikishia nafasi ya kwanza - kama hali ilivyokuwa wakati Benedict alipochaguliwa kuwa Baba Mtakatifu mwaka 2005 baada ya kifo cha Papa Yohanne Paulo II.
Hata hivyo, pamoja na majina mbalimbali kutajwatajwa, Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson amechomoza kuwa chaguo la mapema akiwa na nafasi ya 5/2, akifuatiwa kwa karibu na Marc Ouellet wa Canada mwenye uwiano wa 3/1.
Ufuatao ni mtazamo wa MailOnline kuhusu wote wanaowania nafasi hiyo, nafasi zao na misimamo yao.

9/4 Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, 64
Nchi: Ghana, Kardinali katika Kanisa Katoliki la Ghana.
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Angependa kuona Papa mwenye ngozi nyeusi. Anaamini kondomu zitumike katika ndoa kama mmoja wao ameathirika na Ukimwi.

5/2 Kardinali Marc Ouellet, 68
Nchi: Canada
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Hakubaliani na utoaji mimba, hata katika kesi za ubakaji.

7/2 Kardinali Francis Arinze, 80
Nchi: Nigeria
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Anaunga mkono uzazi wa mpango na utoaji mimba.

7/1 Askofu Mkuu Angelo Scola, 71
Nchi: Italia
Alipandishwa daraja na Papa Benedict XVI kuwa Askofu Mkuu wa Milan.
Misimamo yake: Anataka kufanya kazi kwa ukaribu kabisa na Waislamu na kutetea Wakristo katika Mashariki ya Kati.

10/1 Kardinali Oscar Rodriguez Maradiaga, 70
Nchi: Honduras
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Kiongozi lakini ni mpinzani wa utoaji mimba.

12/1 Kardinali Tarcisio Bertone, 78
Nchi: Italia
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Alikemea vikali vitendo kunajisi watoto wadogo vinavyofanywa na mapadri wa Katoliki na mapenzi ya jinsia moja.

14/1 Kardinali Angelo Bagnasco, 70
Nchi: Italia
Alipandishwa daraja na Papa Benedict XVI kuwa kardinali.
Misimamo yake: Alipingana vikali na utoaji mimba na kuonesha wazi hasira dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

16/1 Kardinali Jorge Mario Bergoglio, 77
Nchi: Argentina
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Alipinga utoaji mimba, pia anapinga ndoa za jinsia moja lakini amehimiza mashoga waheshimiwe. Aliosha miguu ya wagonjwa wa Ukimwi 12 mwaka 2001.

20/1 Kardinali Leonardo Sandri, 69
Nchi: Argentina
Alipandishwa daraja na Papa Benedict XVI kuwa kardinali.
Misimamo yake: Alisema Wakristo nchini Irak chini ya Saddam Hussein walikuwa huru zaidi kuliko walivyo sasa.

25/1 Kardinali Christoph von Schonborn, 68
Nchi: Austria
Alipandishwa daraja na Papa Yohanne Paulo II kuwa kardinali.
Misimamo yake: Alisema matumizi ya kondomu kwa walioathirika na Ukimwi yanaweza kuonekana kama 'dhambi ndogo'.

50/1 Askofu Mkuu Vincent Nichols
Nchi: England na Wales
Aliteuliwa kama Askofu Mkuu wa Westminster April, 2009
Misimamo yake: Alijaribu kuepusha wakala wa Katoliki dhidi ya kuwaweka watoto na mashoga lakini alionekana kukubaliana zaidi na ndoa za jinsia moja.

1 comment:

Anonymous said...

http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/http://www.ryansloans.co.uk/You should be а part of a contest for onе of the
most useful sites on the net. I most certаinlу wіll highly гecommend thiѕ web site!


Ηere is my web pagе; payday loans bad credit
My site ... %anchor_text%