Sunday, February 3, 2013

JAJI BABU ALIYEATHIRIKA NA PICHA ZA NGONO ASIMAMISHWA KAZI KWA SIKU 60...

KUSHOTO: Joseph Polito. KULIA: Mahakamani ambako shauri hilo lilisikilizwa.
Jaji wa Illinois ambaye alikiri kuwa ameathirika na picha za ngono amesimamishwa kwa siku 60 bila malipo kwa kutumia kompyuta yake ya mahakamani kutembelea zaidi ya tovuti 200 za ngono.
Hukumu ya Ijumaa iliyotolewa na Kamisheni ya Mahakama za Illinois imekuja miezi mitatu baada ya Jaji wa Mahakama ya Will, Joseph Polito mwenye miaka 69 huku akibubujikwa machozi kukiri kwamba ameathirika kwa kipindi kirefu maishani mwake na ngono.
Aprili mwaka jana, gazeti la Chicago Sun-Times lilibainisha kwamba jaji huyo mara kwa mara alikuwa akitazama picha chafu kwenye tovuti kadhaa za ngono kati ya nyingine nyingi, wakati wa saa za kazi kati ya mwaka 2010 na 2011.
Katika uamuzi wake, kamisheni hiyo iliandika kwamba tabia ya sehemu ya kazi ya Polito kwa kiasi kikubwa 'haikubaliki,' lakini ilikubali ukweli kwamba mtu huyo mwenye miaka 69 alikuwa ameathirika na dawa za kulevya au pombe, gazeti la Chicago Sun-Times liliripoti.
Ingawa imegulika kwamba utazamaji wa Polito wa picha za ngono kwenye sehemu yake kati ya usikilizwaji haukuwa na athari zozote kwa ubora wa kazi yake, kamisheni hiyo ilinukuu kwamba wakati majaji wanabeba ongezeko kubwa la mizigo ya kesi, vitendo vyake vilikuwa 'upotezaji mkubwa wa muda wa kesi ambao hauvumiliki.'
Polito, ambaye amekuwa jaji mshiriki tangu mwaka 2006, anaweza kukabiliwa na adhabu kali zaidi kuwahi kupata, hajasema lolote kuhusu uwezekano wa kujiuzulu pale kipindi chake kitakapomalizika katika miaka miwili na nusu ijayo.
Mwanasheria wa Polito, William J. Martin, alilieleza Sun-Times Ijumaa kwamba mteja wake ameelezea kifungo chake cha miezi miwili kama 'uamuzi sahihi wa kesi yenye kuvuta hisia za wengi.'
Uchunguzi kwenye kompyuta iliyotumika yenye akaunti ya Polito umeanza baada ya uhuru wa maombi ya taarifa kuwa umewasilishwa  na ChicagoSun-Times.
Mwanzoni Jaji Mkuu Kinney akikataa kukabidhi kumbukumbu - na alisema kwamba taarifa zilikuwa 'kumbukumbu za mahakama' na hazikutakiwa kuanikwa hadharani.
Hatahivyo, nyaraka hizo baadaye ziliwekwa hadharani baada ya Mwanasheria Mkuu wa Illinois kusema kwamba orodha ya tovuti za ngono zilikuwa 'hazihusiani na shughuli zozote za mahakama [na] si za kumbukumbu za mahakama."
Taarifa hizo zilizowekwa hadharani ni za kipindi cha miezi sita takribani mwisho wa mwaka 2010.
Kutoka kwenye akaunti ya kompyuta ya Polito alikuwa ameweza kufungua tovuti 243 tofauti za ngono katika siku tano tofauti.
Wakati huo, Polito alikuwa amehusishwa kwenye kesi ndogo za madai, kesi za magari na kesi za utwaliwaji wa mali.
Wakati wa usikilizwaji wa kesi yake Novemba, Polito aliangua kilio mbele ya kamisheni hiyo, akiomba radhi kwa tabia yake na kubainisha kwamba kuathirika kwake na ngono kulianza wakati alipokuwa na miaka minane tu.
"Nilitumia picha cha ngono kushughulika na hisia zangu za mapungufu," aliongeza wakati wa usikilizwaji kesi hiyo. "Kwa miaka 60 hii ilikuwa vurugu yangu ya ndani - nilikuwa nikiona haya, sikuwa nikijisikia vizuri kwa hili na nilijaribu kuacha. Njia pekee niliyofahamu kulielezea ilikuwa kwenye maungamo nikiwa na mchungaji."
Polito alisema wakati huo kwamba alisaka msaada wa kitaalamu kwa ajili ya matatizo ya hiari ya ngono na kwamba alihudhuria mikutano isiyofahamika la masuala ya ngono, akitoa wito kwamba hakuwahi kutembelea tovuti za ngono kwa zaidi ya mwaka.
Adhabu hiyo ya kusimamishwa Polito inaanza rasmi Februari 16, mwaka huu.

No comments: