![]() |
| KUSHOTO NA KULIA: Muhammad Ali akiongozwa na mkewe, Lonnie kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya London 2012. KATIKATI: Muhammad Ali miaka michache iliyopita. |
Bondia mkongwe Muhammad Ali anaumwa sana kiasi kwamba anaweza kufariki ndani ya siku chache, kaka yake ametahadharisha.
Rahman Ali alisema bingwa huyo wa zamani wa ngumi za uzito wa juu hawezi kuongea na hawezi tena kumtambua.
Rahman anahofia kaka yake huyo mwenye miaka 71 - anayefahamika kama The Greatest - hawezi kufika kipindi kijacho cha majira ya joto.
Alilieleza gazeti la The Sun: "Yuko katika mwelekeo mbaya. Anaumwa sana.
"Inaweza kuwa miezi michache, inaweza kuwa siku kadhaa. Sifahamu kama anaweza kufika kipindi cha majira ya joto. Yuko kwenye mikono ya Mungu."
Ali aligundulika kuwa na maradhi ya kiharusi mwaka 1984 lakini ameendelea kudumu kwa miaka mingi na kujitokeza kwenye Michezo ya Olimpiki ya Atlanta mwaka 1996 ambako aliwasha mwenge.
Hatahivyo, alionekana amekonda na dhaifu kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki mjini London 2012 ambako alisaidiwa na mkewe, Lonnie kwenda jukwaani.
Rahman amemtuhumu shemeji yake, ambaye alifunga ndoa na Ali miaka 26 iliyopita, kwa kukataa kuiruhusu familia yake kumtembelea bingwa huyo anayeugua.
Rahman, ambaye pia ni bondia wa kulipwa, alisema mara ya mwisho alimwona kaka yake Julai katika maonesho ya Sports for Peace mjini London na aliruhusiwa tu kuongea naye kwa njia ya simu.
Makaka hao, ambao majina yao ya kuzaliwa ni Cassius na Rudolph Clay, walikua pamoja huko Louisville, mjini Kentucky.
Hofu ya hali mbaya ya Ali hivi karibuni ilikuwa Desemba, 2011, wakati bingwa huyo alipokimbizwa hospitali baada ya kuwa amepoteza fahamu.
Watu wa huduma za dharura waliitwa siku chache baada ya Ali kuonesha kudhoofika wakati wa mazishi ya bindia mwenzake, Joe Frazier.
Alitibiwa tatizo la upungufu wa maji baada ya kuanguka kwenye shamba lake lenye ukubwa wa futi za mraba 6,000 mjini Arizona.
Rahman alilieleza The Sun kutoka kwenye ghorofa lake mjini Louisville kwamba kabla hali ya Ali kuzorota, alisema alikuwa hana maumivu na alikuwa akijivunia maendeleo yake mazuri.
Rahman, ambaye aliwahi kupata maradhi ya kupooza katika maisha yake ya masumbwi, alisema anajihisi kufadhaishwa kuondolewa katika maisha ya kaka yake, ambaye amemlinganisha na Yesu, ambaye anasema anawapenda wote.
Alisema: "Unafahamu neno 'Isiyo na kikomo'? Huyo ni Ali, yeye hana kikomo. Jina lake litadumu milele."
Baba wa watoto tisa, Ali anataka Nukuu ya Martin Luther King kwenye kaburi lake, kwa mujibu wa Rahman.
Nukuu hiyo ni: "Nilijaribu kumpenda fulani, nikajaribu kumshibisha mwenye njaa.
"Nilijaribu, katika maisha yangu, kuwavika wote waliokuwa uchi. Nitakutaka useme kwamba nilijaribu kupenda na kuhudumia utu." The Greatest."
Mke wa Ali alikataa kutoa maoni yake kuhusu madai hayo ya Rahman.

No comments:
Post a Comment