![]() |
| KUSHOTO: Mama Teresa ambaye ni miongoni mwa wanawake 15 waliopata tuzo ya amani ya Nobel mpaka sasa. KULIA: Malala Yousafzai. |
Mwanafunzi wa kike wa Pakistani ambaye alipigwa risasi na wafuasi wa kundi la Taliban baada ya kuwashutumu hadharani ametajwa kuwania Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu.
Malala Yousafzai mwenye umri wa miaka 15, alipendekezwa na wabunge watatu wa Norway, ambao walienzi "kuthubutu kwake kulikowatisha watu hao wenye siasa kali kwamba walijaribu kumuua'.
Freddy de Ruiter, kutoka chama tawala cha nchi hiyo cha Labor, alisema ujasiri wake katika kuongea hadharani, hasa kuhusu haki za wasichana kupata elimu, kumemfanya awe mgombea mwenye thamani kubwa.
Gorm Kjernli alisema kwenye tovuti ya chama hicho juzi kwamba msichana huyo "ameleta hamasa kubwa kwa dunia nzima."
Aliongeza: "Anawakilisha kizazi cha vijana kinachotumia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe wao kuhusu haki za wasichana katika haki sawa."
Wabunge hao watatu wamewasilisha mapendekezo yao kwa Kamati ya Tuzo za Nobel nchini Norway.
Magne Rommetveit alisema Malala kwa sasa ni 'alama muhimu katika mapambano dhidi ya nguvu za uvunjaji ambazo zitalinda demokrasia, usawa na haki za binadamu."
Malala alipigwa risasi kichwani na mfuasi wa Taliban aliyekuwa na bunduki akiwa karibu kabisa wakati akiwa anasafiri kwenda nyumbani kutoka shule kwa kutumia basi Oktoba 9.
Mshambulizi wake alikuwa kwenye gari huko Swat Valley nchini Pakistani na kumhoji binti huyo kwa kumtaja jina kabla ya kumfyatulia risasi tatu mbele ya rafiki zake walioingiwa hofu kubwa.
Aliunguzwa baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii akishutumu vikali taasisi ya Waislamu.
Malala alikimbizwa hospitali nchini Uingereza wiki moja baadaye, na sasa anafanyiwa upasuaji mkubwa kupachika kipande maalumu cha bati kwenye tundu upande wa kushoto kwenye fuvu lake.
Ameshapokea maelfu ya meseji kutoka kwa watu mbalimbali wanaomtakia afya njema kote duniani, na kuendelea kuzungumza kwa niaba yake.
Msichana huyo mwenye miaka 15 kwa sasa ni alama inayotambulika kimataifa ya upinzani dhidi ya vitendo vya Taliban kupiga vita elimu ya wanawake, na dhidi ya wenye msimamo mkali wa kidini katika nchi hiyo ambako haki za wanawake zimezimwa kabisa.
Kristian Berg Harpviken, mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Oslo: "Tuzo kwa Malala haitokuwa ya muda tu na kutoshea katika mstari wa tuzo kwa mabingwa wa haki za binadamu na demokrasia, lakini pia … itawaweka watoto wote na elimu katika amani na agenda ya migogoro."
Upendekezwaji huo bado haujatangazwa rasmi, lakini juzi ilikuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha majina. Mshindi atatangazwa hadi kufikia mwanzoni mwa Oktoba.
Uchaguzi unaweza tu kufanywa na kundi la watu waliochaguliwa kote duniani, na taasisi hiyo haijataja majina ya wanaowania tuzo hadi miaka 50 baadaye, ingawa wote wanaotaja majina ya wagombea hao wakati mwingine huwataja hadharani.
Mshindi mwenye umri mdogo kabisa kati ya washindi 93 ambao wameshatunukiwa tuzo hiyo alikuwa Tawakkol Karman, ambaye alipokea mwaka 2011, akiwa na miaka 31 wakati huo.
Wastani wa umri wa Tuzo za Amani za Nobel kati ya mwaka 1901 na 2011 ni miaka 62. Kumekuwa na wanawake 15 tu waliowahi kushinda tuzo hizo, ambao ni pamoja na Mama Teresa na Aung San Suu Kyi.
Taasisi Nobel yenye makazi yake mjini Stockholm ilisema majina 231 yalipendekezwa mwaka jana kwa ajili ya kuwania tuzo hizo za amani, ambazo zitakabidhiwa mjini Oslo, Norway.
Wengine wanaofahamika kuwa wametajwa kuwania tuzo hizo mwaka huu ni wanaharakati wa haki za bianadamu ambao majina yao yalitajwa katika miaka iliyopita, akiwamo Belarussian Ales Belyatski - kwa sasa anatumikia kifungo - na Lyudmila Alexeyeva wa Urusi.

No comments:
Post a Comment