Saturday, February 2, 2013

ALIYEFIA NYUMBANI KWAKE AGUNDULIKA BAADA YA MIAKA MIWILI...

KUSHOTO: Eneo la Brighton ambako alikuwa akiishi Simon. KULIA: Simon Allen.
Mtu anayeishi pekee amekufa na mwili wake kubaki ndani ya ghorofa lake lililoko katikati ya jiji kwa miaka miwili baada ya kutokuwapo na yeyote aliyegundua kuwa amefariki, imeelezwa.
Mabaki ya mifupa ya mwili wa Simon Allen yaligunduliwa pale wafagiaji walipokwenda nyumbani kwake kwa lengo la kufanya usafi.
Mwili wake - uliokuwa na jozi moja tu ya soksi - ulikutwa umelala nyuma ya kiti katika sebule ya ghorofa hilo lililoko huko Brighton, mjini East Sussex, Novemba mwaka jana.
Siku 11 kabla mwenye nyumba wake na maofisa wa mahakama walifika kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo hilo kufuatilia kwanini kodi yake haijalipwa kwa miezi kadhaa.
Majirani walisema kulikuwa na 'hafuru kali' kwenye njia iliyoko mbele ya jengo hilo kabla mwili wake kugundulika, lakini hakukuwa zaidi na kingine kisicho cha kawaida kuliko hicho.
Polisi walisema waliamini kwamba Simon alifariki Desemba, 2010 wakati huo alipokuwa na umri takribani miaka 50.
Hawakuweza kupata mwanafamilia yeyote au marafiki na walikuta vitu vichache binafsi katika ghorofa hilo, ambalo Simon alipanga tangu mwaka 1999.
Paul Hanscomb, mwenye miaka 45, ambaye anaishi katika ghorofa ya chini alisema: "Sikuwahi kumuona kwa takribani miaka miwili hivi.
"Alikuwa mlevi mno na nilikuwa nikimsikia akigonganje ya jengo na wakati akipanda ngazi  wakati anaporejea nyumbani usiku.
"Lakini wote tulibaki nayo moyoni hapa na tulidhani kuwa ameondoka."
Chris Dunbar, ambaye pia anaishi ghorofa ya kwanza, aliongeza: "Ilikuwa mshituko mkubwa.
"Nafikiri hakika ni huzuni kubwa na pengine uchunguzi unatakiwa kufanywa mapema kidogo."
Alisema kulikuwa na harufu kali kidogo mbele ya jengo hilo kabla ya mwili wa Simon kugunduliwa.
Uchunguzi wa kisheria wa Brighton umeelezwa kwamba Simon alikuwa akilala kwenye viti viwili vilivyobananishwa na alikuwa akitumia chumba chake cha kulala kwa ajili ya kuhifadhia vitu.
Affinity Sutton, umoja wa upangishaji ambao unamiliki ghorofa lake, ulisema alikuwa 'mpangaji wa mfano'.
Tracy Evans, mkuu wa upangishaji eneo la kusini wa Affinity Sutton, alisema: "Tumehuzunishwa mno kusikia kifo cha Simon.
"Hakukuwa na dalili zozote kwamba kulikuwa na matatizo wala kwamba alikuwa akihitaji msaada wa ziada na alikuwa mpangaji wa mfano.
"Kwa majonzi, licha ya kujaribu kuwasiliana na Simon, hakukuwa na ishara yoyote hadi pale malimbikizo ya kodi kuwa makubwa hadi kufikia mwaka 2012."
Polisi walisema hakukuwa na mshukiwa yeyote kuhusiana na mazingira ya kifo chake na haikuwa rahisi kuelezea jinsi alivyokufa.
Simon alipatiwa huduma ya maziko, inayotolewa kwa watu ambao hawana familia zinazojulikana au marafiki wa kuandaa mazishi yao au uchomaji wa miili yao.

No comments: