![]() |
| Ndege hiyo baada ya kutua Uwanja wa Ndege mjini Denver. |
Abiria mkaidi alipandwa na hasira pale msafiri mwenzake alipohamishwa kwenda viti vyathamani ya juu bila kulipa chochote sababu televisheni ya kwenye ndege ya mtu huyo ilikuwa imevunjika.
Mwanamke mwenye miaka 42 aliyekuwa kwenye ndege ya JetBlue kutoka Uwanja wa John F. Kennedy mjini New York kwenda San Diego alimvamia mhudumu wa ndege kutokana na kutotenda haki, na hivyo kulazimisha ndege hiyo kubadili uelekeo na kwenda Denver majira ya Saa 1:15 usiku (Saa za Marekani) wa Alhamisi.
JetBlue imesema baada ndege namba 185 kutua mjini Denver, mwanamke huyo alikutana na maofisa wa kusimamia sheria.
Shirika hilo la ndege limesema abiria 137 walikuwamo katika ndege hiyo na waliendelea na safari yao masaa kadhaa baadaye.
Abiria waliieleza televisheni ya KMGH mwanamke huyo alikuwa ameketi kwenye kiti namba 2D, kwenye sehemu ya gharama ya juu, ndipo abiria mwingine alipohamishiwa kwenye sehemu hiyo sababu televisheni yake haikuwa ikifanya kazi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mwanamke huyo alipandwa na hasira kwamba mtu huyo alihamishiwa kwenye sehemu yake ya thamani ya juu bila kuongeza malipo na akaingia katika malumbano na mfanyakazi wa ndege hiyo hadi kufikia kukunjana.
Wasimamizi wa sheria walisema mwanamke huyo akawa "akifoka na alikuwa akijichanganya na wafanyakazi wa ndege hiyo."
Jemedari wa shirikisho la anga akaingilia kati na ndege hiyo ikabadili uelekeo.
Polisi wa Denver wamesema hawatafungua mashitaka.

No comments:
Post a Comment