Wanandoa wameshitakiwa kwa udhalilishaji mtoto baada ya kudaiwa kujaribu kumpunga upepo binti yao wa miaka 10, ambaye walikuwa wakifikiri ni mchawi.
Wawili hao, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), walishitakiwa Ijumaa mjini Boraas, magharibi mwa Sweden.
Daniel Larson, mwendesha mashitaka wa serikali, alisema wanandoa hao 'wanafikiri binti yao ni mchawi na kukanusha madai' ya udhalilishaji, kwa mujibu wa gazeti la the Telegraph.
Wanadaiwa kutenda makosa matatu ya udhalilishaji yaliyofanyika kati ya Februari 2007 na Februari 2008, ikiwamo kumlazimisha binti huyo kunywa mchanganyiko wa dawa ya kusafishia na mkojo wake mwenyewe.
Pia walidaiwa kumpiga binti huyo hadi akawa hajitambui.
Mtoto huyo, ambaye anadaiwa kuwa si wa kuzaliwa na wazazi hao, alipelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto mwaka 2008 baada ya hofu taarifa kwamba alikuwa akiteswa nyumbani hapo.
Walimu wake walikuwa wakihofia kuhusu nguo zake chafu, na kuhisi kwamba alikuwa akichukuliwa tofauti na kaka na dada zake.
Daniel alisema ilikuwa baada tu ya kuondolewa kutoka kwa wazazi wake kwamba akaanza kujisikia salama vya kutosha kuhusu uzoefu wake alioupata siku zilizopita.
Gazeti la Boraas Tidning limeripoti mtandaoni kwamba mwaka 2008, wazazi hao waliomba serikalini pesa ili kumrejesha binti huyo nchini DRC kwa ajili ya kupunga upepo, ingawa maombi hayo yalitupiliwa mbali.
Hukumu ya kesi hiyo itatolewa katika miezi michache ijayo.

No comments:
Post a Comment