Saturday, January 5, 2013

WAHOFIWA KUFA BAADA YA CHOMBO CHAO KUZAMA ZIWA TANGANYIKA...

Habari zilizotufikia zinasema kuwa watu kadhaa wanahofiwa kufa maji baada ya chombo walichokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Tanganyika karibu na kijiji cha Herembe, wilayani Uvinza, mkoa wa Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo bado hazijathibitishwa, imedaiwa kwamba hadi jana usiku tayari maiti nane za wanaosadikika kuwa abiria wa chombo hicho zilikuwa zimeshaopolewa. Haikuelezwa jinsia za miili ya watu hao.
Haikuweza kufahamika mara moja uelekeo wa wapi kilipokuwa kikitoka chombo hicho wala kilipokuwa kikielekea licha ya kuelezwa kwamba chanzo cha ajali hiyo kwa mujibu wa taarifa za awali kuwa ni mawimbi makubwa. Pia aina na idadi ya watu waliokuwamo katika chombo hicho havikuweza kupatikana mara moja.
Habari kamili kuhusu ajali hiyo utazipata hapahapa baadaye
.

1 comment:

Anonymous said...

thank you for info.which made me to be alerted on that worse situations in lake tanganyika where ibelong.
my suggestion is keep on alerting various information because nobody write on that remote area like Herembe and other areas like that.Do not relies on the events only but even other events keep on reporting for the best of your knowledge.
thank you its me kalimanzila J H