Saturday, December 8, 2012

RIPOTI YA UCHUNGUZI MPYA WA MWILI WA NOTORIOUS BIG HAYA HAPA...

Christopher Wallace "Nororious BIG" alipatwa majeraha ya risasi kifuani, begani, mguuni, kiganjani na kwenye korodani katika usiku ambao aliuawa mjini Los Angeles mwaka 1997 ... hii ni kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi ambayo haiwahi kuonekana hapo kabla, ambayo imepatikana.
Ripoti hiyo imethibitisha Wallace alishambuliwa mara nne katika shambulio la bunduki huko Wilshire Blvd wakati rapa huyo mwenye miaka 24 akiwa ameketi kwenye kiti cha abiria ndani ya gari aina ya Chevy Suburban.
Ripoti inasema ... baada ya risasi ya pigo namba tatu kutoka katika paja, mvurumisho huo ukashambulia nyonga ya upande wa kushoto wa korodani, na kusababisha kina kifupi, mkwaruzo unaofifia wa inchi 3/8."
Risasi mbaya zaidi ilikuwa ya pigo namba nne ... ambayo iliingia mwilini mwa Wallace kupitia nyonga yake ya kulia na kupenya kupitia viungo kadhaa nyeti ... kabla ya kutua kwenye eneo la bega lake la kushoto.
Kwa mujibu wa ripoti, risasi hiyo ilitoboa utumbo mpana wa Wallace, ini, moyo na sehemu ya juu ya pafu lake la kushoto.
Mara baada ya kushambuliwa huko kwa bunduki Wallace alikimbizwa Hospitali ya Cedars-Sinai ambako madaktari walimfanyia huduma ya dharura ... lakini walikuwa wamechelewa mno. Wallace alitangazwa kufariki dunia majira ya Saa 7:15 usiku wa manane.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mara zote nne risasi zilipenya kupitia mlango wa abiria wa gari hilo aina ya Suburban kabla ya kumpata Wallace. Risasi mbili zilikutwa kwenye gari lililompeleka Wallace hospitalini. Risasi nyingine iligunduliwa katika hospitali wakati mwili wake ulipogeuzwa baada ya madaktari kutangaza kwamba amefariki.
Wakati uchunguzi ukiendelea Wallace alitajwa kama 'mwenye unene wa kuchukiza.' Kipimo cha sumu kilibainisha kwamba Wallace hakugundulika na dawa zozote za kulevya au pombe katika mfumo wake wa damu wakati wa kifo chake.
Mwili wa Wallace kisha ukapelekwa kwa mama yake na mke wake kwa ajili ya utambuzi.

No comments: