Mganga wa jadi katika kijiji cha Ng’ombe, Kata ya Nyamagoro, Tarafa ya Nyancha wilayani Rorya katika Mkoa wa Mara, ameuawa kikatili kwa kuchomwa mkuki kiunoni upande wa kushoto na kukatwakatwa mapanga kichwani na mgonjwa wa akili aliyekuwa akimtibu kijijini hapo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Tarime/Rorya, Justus Kamugisha alisema ofisini kwake jana kuwa watu wawili wameuawa kikatili juzi baada ya mganga wa tiba za asili, Mang’era Makori (48), kushambuliwa kwa kuchomwa mkuki kiunoni upande wa kulia na kukatwakatwa mapanga kichwani na mgonjwa aliyekuwa akimtibu ugonjwa wa akili, Abichi Jeremiah (36) nyumbani kwake kijijini hapo.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wenye hasira wa kijiji hicho waliamua kujichukulia sheria mikononi na kumwadhibu mgonjwa huyo wa akili kwa kumshambulia kwa kipigo sehemu mbalimbali za mwili wake wakitumia silaha za jadi mpaka kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema mganga Mang’era alifikwa na mkasa huo saa tatu asubuhi wakati akiendelea kuwapatia huduma ya matibabu wateja wake na kwamba mgonjwa huyo wa akili alipelekwa nyumbani kwake kutibiwa ndipo alipomvamia mganga aliyekuwa akijaribu kumsaidia matatizo ya akili na kusababisha kifo chake.
Kamanda Kamugisha alisema, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusu mauaji hayo na kwamba polisi mkoani hapa wanaendelea uchunguzi wa matukio.

No comments:
Post a Comment