CHEKA TARATIBU...

Mwalimu wa darasa kaingia darasani na kuuliza, "Nani kamuua Chifu Mkwawa?" Mtoto wa kwanza akajibu, "Mi sijui, jana sikuja shule!" Mtoto wa pili akajibu, "Mi jana nilitoka mapema, sijui kilichotokea!" Mwalimu kwa hasira akaenda kuripoti kwa mwalimu mkuu. Mwalimu Mkuu akaenda kwenye lile darasa na kuwauliza wanafunzi swali lile na majibu yakawa yale yale. Walimu wakatoka nje, ndipo Mwalimu wa Darasa akamuuliza bosi wake, "Hivi una hakika muuaji yuko kwenye darasa langu?" Duh…

No comments: