Sunday, November 11, 2012

O.J. SIMPSON AJA KIVINGINE KUJARIBU KUTOKA GEREZANI...

O.J. Simpson katika nyakati tofauti mahakamani.
Jaji wa Nevada amekubali kumruhusu O.J. Simpson kuthibitisha kwa mara ya kwanza kuhusiana na ushiriki wake katika ujambazi wa kutumia silaha huko Las Vegas ambao ulimsababisha hukumu ya kifungo cha muda mrefu jela.
Shauri hilo limepangwa kusikilizwa Mei 13, mwakani na linaweza kuibua ushahidi mpya kwamba hukumu yake ikapitiwa upya.
Nyota huyo wa zamani wa mpira wa miguu anatarajiwa kuthibitisha kwamba aliwakilishwa vibaya na mwanasheria wake na kwamba anatakiwa kushitakiwa upya kwa msaada wa jopo lililo bora zaidi.
Mwaka 2008, Simpson alihukumiwa kutumikia kifungo cha kati ya miaka tisa na 33 gerezani, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuongoza watu watano katika tukio la ujambazi wa kutumia silaha.
Simpson alikuwa akituhumiwa kuwapora wafanyabiashara wawili wa michezo na dalali wao katika Hoteli ya Las Vegas and Casino.
Simpson alisisitiza kwamba alikuwa akijaribu kurejesha baadhi ya vitu vyake binafsi ambavyo viliibwa baada ya kuachiliwa mwaka 1995 katika tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mkewe, Nicole Brown Simpson, na rafiki yake, Ronald Goldman.
Pia alieleza kwamba hakuwa akifahamu mtu aliyepeleka bunduki usiku huo wa tukio.
Pingamizi la Simpson linadai kwamba mwanasheria wake, Yale Galanter, hakutakiwa kuruhusiwa kumwakilisha. Si tu kwamba Galanter alifahamu kuhusu tukio la 2007 kabla halijatokea, alibishana, alishiriki kusaidia Simpson kulipanga.
Mwanasheria huyo, hatahivyo, alikanusha kwamba alikuwa na ufahamu wowote kabla ya tukio na alimweleza jaji kwamba 'hakuwapo eneo hilo' na 'hakuwa na chochote cha kufanya' kukabiliana nalo.
Pingamizi hilo pia linasema kwamba Galanter alificha taarifa, ambazo zingeweza kumfanya Simpson apate hukumu ya muda mfupi zaidi. Kwa uhakika zaidi, Simpson anadai kwamba Galanter hakumweleza makubaliano ya kabla ya hukumu kwamba ingeweza kumfunga kwa miaka miwili hadi mitano.
Simpson alisema kama angelijua kuhusu makubaliano hayo, basi angekuwa ameshaafikiana nalo kutumikia.
Tangu kesi hiyo, Galanter amekumbana na mashambulio kutoka pande zote. Kwa kuongezea kwenye madai yaliyozushwa dhidi yake na Simpson, Galanter pia anashitakiwa na mwanasheria mwenzake wa zamani, Gabriel Grasso kwa kuvunja mkataba.
Katika kulipa kisasi, Galanter amefungua mashitaka ya upotoshaji dhidi ya Grasso, mwanasheria wake na wanasheria wa zamani wa Simpson katika kesi ya pingamizi.
Simpson amemuweka kando kabisa Grasso kwenye pingamizi lake.

No comments: