![]() |
| KUSHOTO: Mwimbaji Usher Raymond akipiga kura Uchaguzi wa Marekani. KULIA: Usher akiwa mbele kabisa ya foleni ya kupiga kura mjini Atlanta. |
Wapigakura mjini Atlanta walipandwa na jazba baada ya Usher Raymond kuvushwa mbele katika foleni na kuwapita watu wengi waliokuwa wametangulia kwenye misululu mirefu siku ya uchaguzi wa Marekani.
Mwanamuziki huyo maarufu anadaiwa kupewa upendeleo maalumu na maofisa wanaosimamia upigaji kura, ambapo aliruhusiwa kuipita foleni ndefu, na wapigakura wenzake hawakufurahishwa na hatua hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vya habari.
Hatahivyo, maofisa wa uchaguzi walisisitiza kuwa Usher aliruhusiwa kusimama mbele ya mstari kuepusha ghasia kutoka kwa umati uliokuwepo mahali hapo.
Walisema katika taarifa kwamba meneja wa kituo hicho cha kupigia kura 'alielekezwa kuhakikisha kwamba uwepo wa (Usher) usiwe chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kuchukua hatua muhimu za kumvusha mbele ya foleni wakati wa zoezi hilo haraka iwezekanavyo.
"Hakukuwa na sababu nyingine yoyote kwa uamuzi wa kumpa upendeleo, ila ni kuepusha vurugu wakati wa zoezi la upigaji kura."
Waliongeza kwamba mwimbaji huyo wa timu ya Climax alikaa mbele kuwataarifu kwamba angeweza kufika hapo kwa ajili ya kupiga kura.
Usher alituma katika mtandano wa Twitter picha yake alipokuwa kwenye kituo cha kupigia kura, akiweka wazi kwamba alikuwa akimuunga mkono Obama.
Aliandika: "Nimepiga kura kwa ajili ya KUSONGA MBELE."
Wakati huohuo, Usher hivi karibuni alitawala vichwa vya habari kwa kutumia Dola za Marekani 12,000 kwa ajili ya kununua mbwa mwingine.
Alikuwa mzabuni wa juu kabisa kwenye mnada wa mbwa huyo katika maonesho ya Pencils of Promise Gala mjini New York mwezi uliopita, ambapo mbwa huyo alinadiwa kwa ajili ya kuchangia fedha za hisani, ambapo zitatumika kujenga shule huko Laos, Nicaragua, Guatemala na Ghana.
Licha ya Usher kufanikiwa kununua mbwa huyo, lakini hapo kabla alikuwa katika wakati mgumu kutoka kwa mzabuni mwenzake nyota wa 'Gossip Girl', Jessica Szohr ambapo alifikia ofa ya Dola za Marekani 11,000 kufuatia ofa ya mwanzo ya Usher mwenye miaka 34 ya Dola za Marekani 10,000.
Utashi wa Usher kununua mbwa huyo uliendelea zaidi na kuongeza dau hadi kufikia Dola hizo 12,000 kabla ya kutupa mikono yake juu katika kusherehekea baada ya kutaarifiwa kwamba mbwa huyo sasa ni mali yake.

No comments:
Post a Comment