Mhalifu mzaliwa wa Algeria anayetuhumiwa kwa 'ndoa kwa ajili ya kitu fulani' kwa raia wa Uingereza amerejeshwa Uingereza kutoka Hispania.
Polisi walisema Lazhari Zemouche ameshakamatwa mara 92 nchini Hispania katika kipindi cha miaka 25 iliyopita kwa makosa ya wizi wa kutumia nguvu na amekuwa akitumia vitambulisho kadhaa vya bandia.
Lakini kwa sababu ameoa nchini Uingereza kabla ya mfululizo wa makosa yake ya hivi karibuni nchini Hispania, alirejeshwa London badala ya kupelekwa kwenye asili yake Algeria.
Maofisa walisema alipandishwa ndege kuelekea London baada ya kukamatwa kwake hivi karibuni mjini Majorca sababu alikuwa akifikiriwa kuwa 'hatari kwa usalama' nchini Hispania.
Vyanzo vya habari vya Polisi Hispania vimedai Zemouche, ambaye mahali aliko hakukujulikana jana usiku, alijiingiza katika ndoa bandia ili kupata pasipoti ya Uingereza.
Walikiri kwamba kama Zamouche asingekuwa akitafutwa nchini Uingereza, angeweza kuwa huru mitaani na kukata rufaa kupinga kama alivyokuwa akifanya kwa zaidi ya karne mbili na nusu zilizopita nchini Hispania.
Kitambulisho cha mke wake na tarehe halisi ya ndoa yake, inayosemekana kufanyika nchini Uingereza 'miaka michache iliyopita', haikuwekwa bayana na mamlaka za Hispania.
Alirejeshwa Uingereza chini ya Sheria ya Hispania ya mwaka 2007 ikiruhusu kutimua raia wa Umoja wa Nchi za Ulaya kwa sababu za kiusalama.
Msemaji wa polisi wa Majorca, ambako Zemouche mwenye miaka 45 alikamatwa Oktoba 4 na kushikiliwa katika kituo cha uhamiaji akingojea kurejeshwa kwao, alikataa kumtaja rasmi jina lake.
Lakini vifupisho vya majina ya Zemouche vimeonekana kwenye magazeti ya nchini humo na kutaarifu vyanzo kuthibitisha utambulisho wake kamili.
Msemaji wa polisi alisema: "Alirejeshwa nchini Uingereza sababu alimuoa raia wa Uingereza nchini humo na ana uraia wa Uingereza.
"Kumbukumbu za polisi zinaonesha alishakamatwa mara 92 tangu mwaka 1987 katika sehemu tofauti za Hispania kwa makosa ikiwamo wizi na ukabaji na ameshawahi kufungwa jela mara kadhaa. Pia ameshawahi kutumia vitambulisho zaidi ya 22."
Chanzo cha habari cha polisi kiliongeza: "Tunahisi alijiingiza katika ndoa za bandia ili kuweza kupata pasipoti ya Uingereza sababu baada ya kuoa alirejea Hispania na kuendelea na utetezi na kwa kawaida hakuonekana kuwa na mawasiliano yoyote na mkewe akiwa Hispania. Kwetu hii ni 'ndoa kwa ajili ya kitu fulani.'
Juzi usiku hakukuwa na majibu yoyote kutoka kwenye anuani ya North London ambako Zemouche alikuwa akidhaniwa kuwa akiishi siku za nyuma.

No comments:
Post a Comment