Tuesday, November 20, 2012

KAKA WA MWIMBAJI AKON AMWOMBA JAJI KUPUNGUZA MADAI YA MZAZI MWENZAKE...

Kaka wa mwimbaji maarufu Akon, Abou Thiam amemtaka jaji kupunguza zaidi madai ya mama mtoto wake … licha ya kuwa na akaunti iliyonona.
Kwa mujibu wa nyaraka za kisheria zilizowasilishwa mahakamani mjini Georgia, Abou alikubali kutoa Dola za Marekani 3,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto aliyezaa na mwanamke huyo, Ariel Hakim mwaka 2010. Wawili hao wana mtoto  mmoja wa kiume.
Lakini Ariel hivi karibuni amewasilisha madai mapya, akiitaka mahakama kumwamuru Abou aongeze kiasi hicho kwa mwezi, akidai kwamba gharama za mtoto zimeongezeka sasa na si hivyo tu, anasema kipato cha Abou kimeongezeka maradufu.
Abou ni Makamu wa Rais wa Def Jam Records na katika nyaraka zilizowasilishwa mwaka 2010 aliorodhesha kipato chake kwamba ni zaidi ya Dola za Marekani 38,000 kwa mwezi.
Abou alitupilia mbali madai hayo ya Ariel Novemba 8, na kuitaka mahakama kupunguza kiasi anachotakiwa kulipa kwa mwezi.
Wakati Abou akilumbana, Ariel amemhamisha mtoto wao huyo kutoka Georgia hadi Florida bila kumpatia notisi ya siku 30 … ambayo anadai imemletea usumbufu katika haki zake za kumtembelea na kumbebesha mzigo mkubwa wa kifedha, ikiwa ni gharama za usafiri.
Anamtaka jaji kuyatosa maombi ya Ariel. Jaji bado hajatoa uamuzi.

No comments: