Saturday, November 17, 2012

MTUHUMIWA UGAIDI AKAMATWA AKIJIANDAA KUTEGA BOMU LIVERPOOL...

KUSHOTO: Raul Sanchez Fuentes Villota. KULIA: Moja ya milipuko ya mabomu iliyofanywa na magaidi wa kundi la ETA mjini Madrid.
Mtuhumiwa wa ugaidi wa ETA anayehusishwa na mauaji kadhaa amekamatwa nchini Uingereza jana baada ya kutafutwa kwa miaka 17.
Raul Sanchez Fuentes Villota mwenye miaka 47, alikamatwa mjini Liverpool kufuatia msako wa pamoja kati ya polisi wa Uingereza na Hispania.
Mtuhumiwa huyo wa ugaidi alikamatwa kwa kibali cha Ulaya kilichotolewa na jaji katika Mahakama Kuu ya mjini Madrid, ambayo inajihusisha zaidi na kesi za ugaidi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema Fuentes alikamatwa Saa 3 asubuhi mjini Liverpool, ambako 'alikuwa akiishi kwa nyaraka za kughushi, akisubiri kupokea maelekezo kutoka kwa uongozi wa kundi la ugaidi la ETA.'
Walisema amekuwa sehemu ya mtandao wa ugaidi wa ETA unaoitwa Matalaz Cell, unaohusika kwa mashambulio kadhaa ya ugaidi nchini Hispania.
Anadaiwa kujiunga na kundi hilo mwaka 1990 na alipewa mafunzo ya kutumia silaha za moto na mabomu.
Matalaz Cell imekuwa ikihusishwa na huduma za usalama Hispania katika mauaji kadhaa.
Wanahusishwa na mauaji ya ofisa wa polisi Jose Manuel Cruz Martin April 1991, ambaye aliuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari mjini Baracaldo.
Alikamatwa akidaiwa kujaribu kufanya mauaji mawili yanayofanana miezi miwili baadaye.
Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema katika taarifa yake: "Kufuatia kutupiana risasi Juni 1991 maofisa kutoka Polisi wa Taifa walimkamata Fuentes na wafuasi wengine wa kundi hilo wakati wakijaribu kutega bomu kwenye gari la ofisa kutoka Polisi wa Taifa mjini Baracaldo."
Fuentes alikamatwa Juni 1991 akidaiwa kujaribu kutega bomu chini ya gari la ofisa wa polisi mjini Baracaldo, huko Vizcaya, jimbo lililoko kaskazini mwa Hispania.
Yeye na wafuasi wengine wawili wa ETA, Juan Maria San Pedro Blanco na German Urizar de Paz, walitupiana risasi na maofisa wa polisi wa Hispania kabla ya kukamatwa eneo la tukio walilopanga kufanya ugaidi.
Fuentes aliachiliwa kwa dhamana Juni 1995 baada ya kushikiliwa kwa miaka minne bila kufunguliwa mashitaka - muda mrefu kuruhusiwa chini ya sheria za Hispania.
Alitoweka miezi miwili baadaye na hati ya kukamatwa kwake ilitolewa Septemba 1995.
Mwaka 2002 polisi waligundua nyaraka zinzzomhusisha Fuentes katika uongozi wa juu wa jeshi la ETA, baada ya kumkamata kiongozi wa juu wa kijeshi wa ETA, Juan Fernandez Iradi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hispania ilisema kayika taarifa yake: "Polisi wa Uingereza kwa kushirikiana na Polisi wa Taifa wameweza asubuhi hii kumkamata mtuhumiwa wa ugaidi wa kundi la ETA, Raul Sanchez Fuentes Villota mjini Liverpool.
"Wapi aliko Fuentes Villota, mtuhumiwa wa mauaji kadhaa, ilikuwa haifahamiki tangu mwaka 1995."
Watuhumiwa kadhaa wafuasi wa ETA wamekuwa wakikamatwa hivi karibuni nchini Uingereza.
Inajumuisha Antonio Troiino, anayehusishwa na mauaji ya watu 22, ambaye alikamatwa mjini Hounslow, magharibi mwa London, mwezi Juni.
Mtuhumiwa mwingine, Benat Atorrasagasti alikamatwa wakati akitoka kwenye baa mjini Edinburgh mwezi uliofuatia.
Na polisi walimkamatwa kiongozi wa STA, Eneko Gogeaskoetxea mwenye miaka 44, katika nyumba moja mjini Cambridge, Julai mwaka jana.
Gogeaskoetxea, aliyekuwa akitafutwa kwa kujaribu kumuua King Juan Carlos mwaka 1997, alikuwa akiishi hapo na mkewe na watoto wawili chini ya jina bandia na pia alikuwa mwanachama wa klabu ya mchezo wa skwashi eneo hilo.
Wataalamu wa kupambana na ugaidi wamesema Uingereza imekuwa chaguo la uhalifu huo kwa magaidi wa ETA baada ya Ufaransa kuanza kushirikiana na Hispania kuwasaka watuhumiwa wanaoishi huko.
Vyanzo kutoka Usalama wa Taifa wa Hispania vimesema kuna takribani magaidi 180 wa kundi la ETA wanaorandaranda humo.
Kundi la ETA limeua zaidi ya watu 800 tangu lilipoanzisha kampeni yake kudai uhuru wa Jimbo la Basque mwishoni mwa miaka 1960.
Januari mwaka jana kundi hilo lilitangaza 'mpango wa kudumu wa kusitisha mapigano' kufuatia zaidi ya miaka 40 ya umwagaji damu.
Kundi hilo la ugaidi limeshauriwa kukabidhi silaha zake na kuwaomba radhi hadharani waathirika wa mauaji hayo.

No comments: