WALIOMTESA VIKALI MWANAUME NA KUMUUA WAFUNGWA MAISHA JELA ...

JUU: Ricky Roys, Andrew Brown na Hellen Cooke. CHINI: Wauaji hao wakipanda basi huku Hellen akionekana kwa nyuma yao. KULIA: Derek Blake.
Watu watatu ambao walimshambulia mwanaume mmoja na kumsababishia majeraha na mateso makali, yanayofanana na yale ya tamthilia ya kutisha ya 'Resident Evil', wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na kifo chake.
Derek Blake mwenye miaka 44 alikutwa amekufa ndani ya bafu lililojaa maji katika ghorofa moja kwenye mji aliozaliwa wa Great Yarmouth, mjini Norfolk, Mei 24 mwaka huu.
Mtaalamu huyo wa elimu ya magonjwa alikabiliwa na majeraha tofauti 104 na alipitia mateso machungu na ya kuumiza mno ikiwamo matumizi ya kisu na nyundo koleo, Mahakama ya Norwich ilielezwa.
Mmoja wa wauaji wake alifananisha baadaye shambulio hilo lililofanyika huku wakiwa wamelewa na tamthilia ya 'Resident Evil', mfululizo wa picha za michezo ya kompyuta ambayo imechangia kutengenezwa filamu tano za kutisha.
Shambulio hilo lilihusisha pia kummwagia Blake maji yaliyochemka kwenye majeraha yaliyotokana na kukatwa na kumuunguza mwili wake wote na kumuumiza na dawa ya kuua wadudu kwenye bwawa la kuogelea.
Herufi J ilichorwa pembeni ya sura yake.
Ricky Roys mwenye miaka 20, Andrew Brown mwenye miaka 42 na Helen Cooke mwenye miaka 19 wote wakazi wa St. Nicholas Road, huko Great Yarmouth, walipatikana na hatia ya mauaji ya mtu huyo.
Jaji Peter Jacobs aliwahukumu wote watatu kifungo cha maisha jela. Brown lazima atumikie miaka 23 jela, Roys miaka 20 na Cooke miaka 18 kabla ya kuanza kufikiriwa kuachiwa huru.
Jacobs alisema: "Hiki ni kifo kilichohusisha vitendo vya ukatili.
"Hii imeenda mbali zaidi ya hukumu kumpiga na kusababisha majeraha haya mengi inathibitisha kwamba mlidhamiria kuua. Mmehukumiwa kutokana na uzito wa vitendo vyenu wenyewe.
"Ni wazi Brown aliongoza lakini hii lazima iwe na uzito sawa dhidi ya kuhusika kwa kila mmoja wenu."
Akifafanua mauaji ya Blake, mwendesha mashitaka Graham Perkins alisema: "Licha ya kumkuta kazamishwa kwenye maji, kifo chake hakikusababishwa na kuzama kwenye maji.
"Alikuwa ni muathirika wa mateso makali kwa zaidi ya kipindi fulani kirefu mno.
Nyundo koleo, kisu cha kuvunjia mifupa na kisu kingine vilikutwa katika ghorofa hilo na hivi vilikuwa vikitumika katika shambulio hilo.
"Inawezekana alibaki hai kwa masaa kadhaa baada ya shambulio hilo. Inawezekana alikuwa mahututi kwa kipindi chote hicyo na inawezekana alikuwa katika maumivu makali sana.
"Uchunguzi wa mwili wake umeonesha kwamba alikufa kutokana na maumivu makali yaliyotokana na mateso na vitendo vya kikatili."
Parkins alisema Blake alikutana na wauaji hao kwenye hosteli mjini humo na wakaanza kunywa pamoja.
Baada ya mauaji hayo, marafiki hao watatu walisimulia shambulio hilo kwa watu waliowafahamu.
Cooke alimwambia mmoja wa mashuhuda: "Tulimkung'uta." Roys alimweleza mwingine: "Ilikuwa kama kwenye filamu ya Resident Evil."
Wakili wa Cooke, Katherine Moore alisema, mteja wake alikuwa na miaka 18 na kwamba alikuwa akiishi na mama yake wakati mauaji hayo yalipotokea.
Aliongeza: "Alikuwa akinywa vibaya sana tangu akiwa na miaka 13. Pia akaja kuacha shule akiwa na umri wa miaka 14."
Mchezo wa Resident Evil wa hivi karibuni 'Resident Evil 6' umeingia mitaani mapema mwezi huu, wakati toleo la tano la mfululizo wa filamu 'Resident Evil: Retribution' kwa sasa inaoneshwa kwenye kumbi mbalimbali za sinema.
Mchezo huo unahusisha kuua maadui kwa kutumia silaha mbalimbali.

No comments: