RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012 KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
1.0
Muhtasari wa ripoti
Ripoti
hii ni ya wa uchunguzi mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa Mwandishi
wa Channel Ten Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo,
wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa Septemba 2, 2012.
Baraza
la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa pamoja
waliunda timu ya uchunguzi.
Mchakato
wenyewe ulihusisha mbinu za uchunguzi za kiuandishi wa habari ambazo si kama za
uchunguzi wa kipolisi na wa kimahakama.
Methodolojia
za uchunguzi zilijumuisha mahojiano, kutembelea maeneo husika na uchambuzi
mahsusi wa nyaraka kwa kuzingatia adidu za rejea zilizopo. Waandishi wa Habari
waliokuwepo Nyololo na ambao hawakuwepo
katika eneo la mauaji wametoa mchango muhimu.
Mashahidi
walioshuhudia katika kijiji cha Nyololo, wakiwemo watoto walikuwa
vyanzo muhimu. Habari zilizochapishwa katika vyombo vya habari kutokana taarifa
rasmi kuhusu baa hilo pia zilichambuliwa kwa umakini.
Uchambuzi
mpana ulifanywa kuhusu hali ya mahusiano ya Uongozi wa Mkoa wa Iringa( ikiwemo
polisi) na wanahabari wa Iringa kabla ya mauaji ya Mwangosi.Mahusiano yalikuwa
si mazuri na ya shaka kati ya pande hizo mbili tangu katika robo ya mwisho ya
mwaka 2011.
Hii
ilisaidia kupata picha pana ya tatizo pamoja na kuweza kufahamu kwa undani
tatizo lenyewe na kuweza kupanga mwelekeo wa uchunguzi wenyewe na hatimaye
kuwezesha timu kuweza kuunganisha mambo na kuandaa ripoti hii.
Aina
nyingine ya ushahidi uliosaidia kuimarisha ripoti hii ni pamoja na video, picha
mgando; maelezo kutoka katika mikutano na waandishi wa habari iliyofanyika
Iringa na taarifa za vyombo vya habari.
Mpaka
wakati ripoti hii inaandikwa, taarifa rasmi kuhusu mauaji ya David Mwangosi
zimekuwa zikitofautiana.
Kwa
kifupi matokeo ya mambo yaliyopelekea mauaji ya Daudi Mwangosi kwanza yanadhihirisha
bila wasiwasi kwamba Polisi kwa makusudi waliwaburuta waandishi waliotoka
Iringa waliokuwa wakifuatlia habari za shughuli za Chadema katika kijiji cha
Nyololo. Zaidi ya hapo, Daudi Mwangosi
mwenyewe aliuliwa akiwa mikononi mwa polisi huku wakiangaliwa
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda.
Uamuzi
huu unadhihirishwa na ushahidi uliokusanywa kwenye maeneo pamoja na video na
taarifa zingine za vyombo vya habari.
2.0
Tamko la Tatizo
Kuanzia
Machi 2012 mahusiano ya kikazi kati ya waandishi wa habari wa mkoa Iringa na
viongozi wa utawala wa mkoa, ikiwemo jeshi la polisi, haukuwa mzuri.
Katika
mikutano yake mbalimbali ya kitaaluma, Klabu ya Waandishi Habari ya Iringa
(IPC) kutoka katika robo ya mwisho mwaka 2011, waandishi wa habari wamekuwa
wakilalamikia “kutotendewa sawa” na maofisa wanapokuwa wakifuatilia na kuandika
habari mkoani Iringa.
Kwa
mfano , Novemba 2011, mwandishi Laurean Mkumbata anayeandikia ITV alipigwa
vibaya na kamera yake ikaharibiwa na aliyekuwa mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya
ya Iringa , wakati mwandishi huyo alipokuwa kazini.
Mkumbata
alieleza mbele ya Timu ya Uchunguzi kwamba yeye na waandishi
wengine , akiwemo marehemu Daudi Mwangosi walikuwa wakikusanya
habari katika mpambano kati ya polisi na kundi moja la watu mjini Iringa. Kundi
hilo lilitaka kuchoma moto nyumba moja iliyodaiwa kuwa na wachawi ambao uwepo
wao ulikuwa ukiathiri eneo lote jirani.
Hali
iliyojitokeza ni kwamba ofisa yule wa polisi alitaka kuharibu kifaa cha kazi
cha mwandishi ili kuzuia upelekaji wa habari kuhusu mpambano wa wananchi wenye
hasira na polisi.
Wakati
polisi walikuwa wakiwadhibiti watu hao kwa kutumia mabomu ya machozi na
kufyatua risasi za moto hewani kuwatisha na kuwaondoa watu hao kutoka eneo la
tukio, OCD Semunyu alimshika mwandishi huyo na kumnyang’anya kamera yake ambayo
aliipiga chini mara tatu, na hivyo kuiharibu kabisa.
Pamoja
na hayo, Mkumbata alishikiliwa kwa muda alipokwenda kutoa taarifa kuhusu tukio
hilo katika makao ya polisi ya mkoa. Baada ya hapo jitihada za kuficha ukweli
zikaanza.
Hata
hivyo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Evarist
Mangala aliingilia kati na kumwamuru ofisa aliyehusika, Semunyu, kulipa kamera
iliyovunjwa. Ofisa huyo alitekeleza amri hiyo na Mkumbata alipata kamera yake.
Ofisa huyo alilipa kutoka mfukoni mwake.
Mkumbata
anaamini kwamba ofisa yule wa polisi aliipiga chini kamera yake mara tatu
kuhakikisha inaharibika kabisa na hakuna kinachopatikana, hatua iliyolenga
kuhakikisha mwandishi huyo hawezi kutangaza taarifa za tukio kwa wakati.
Tangu
wakati huo hali ya kutiliana shaka imekua katika mahusiano ya wanahabari wa
Iringa na Polisi. Mahusiano na viongozi wengine wa mkoa nayo hayajakuwa mazuri
tangu kipindi hicho cha robo ya mwisho ya 2011.
Frank
Leonard, Katibu wa IPC anakumbuka kuwa mwishoni mwa Februari
2012, waandishi saba waliteuliwa na IPC kuandika habari ya ziara ya Makamu wa
Rais mkoani Iringa, lakini walilazimika kulala ndani ya basi walilosafiria kwa
kuwa maofisa wahusika wa mkoa walidaiwa kupuuza kuwapatia hoteli ya kulala.
Tukio
hilo liliudhi uongozi wa IPC ambao uliandaa maandamano ya amani kulalamikia
unyanyasi wa waaandishi wa habari unofanywa na viongozi wa mkoa.
Hatua
hiyo, kwa mujibu wa Katibu huyo ililenga kuwasilisha kwa viongozi wa mkoa
msimamo kwamba “Wanachama wa IPC hawaegemei chama chochote cha siasa, bali ni
wanataaluma na wanaosimamia uandishi habari unaozingatia maslahi ya umma”.
Machi
6, 2012, mamlaka ya polisi ya mkoa uliidhinisha ombi la IPC kuandamana
kupinga kuendelea mahusiano yasiyo mazuri kati ya waandishi
wa habari na uongozi wa mkoa.
Katibu
wa IPC anakiri kwamba mahusiano kati ya
pande hizo mbili yaliboreka
baada ya maandamano hayo ambapo aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa aliahidi
kushughulikia tofauti zilizopo na kuhakikisha kunakuwa na maelewano.
Kubadilika
kwa mambo ghafla na kufikia mauaji ya Daudi Mwangosi hapo Septemba 2,
2012, wakati a akikusanya habari za shughuli za kisiasa za Chadema katika
wilaya ya Mufindi , katika kijiji cha Nyololo mikononi mwa polisi wanaotuhumiwa
kwa mauaji inastusha na ni jambo lisilo la kutegemewa kwa Frank Leaonard.
Marehemu Daudi Mwangosi alikuwa Mwenyekiti wa IPC.
3.0
Mamlaka
Mamlaka
ya uchunguzi huu inatokana na katiba ya Baraza la Habari Tanzania
(MCT), kifungu 3 (e), kinachoelezea malengo ya Baraza kuwa ni:
Kuwa
na rejista ya matukio yanayoweza kukwaza upatikananji wa habari za manufaa kwa
umma na muhimu, na kuchunguza tabia za watu, mashirika na vyombo vya serikali
kwa ngazi zote dhidi ya vyombo vya habari, na kutangaza matokeo ya uchunguzi
huo.
3.1
Lengo
Lengo
la uchunguzi huo ni kuweka rekodi sawa ya mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa
mwandishi wa Channel Ten na Mwenyekiti wa IPC, David Mwangosi , Septemba 2,
2012 katika kijiji cha Nyololo , wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa .
Uchunguzi
huo ni huru na sio kama wa kipolisi au wa kimahakama lakini ni jitihada za
dhati za kuweka kumbumbuku ya hali ya mambo kuhusu kifo cha kwanza cha
mwandishi wa Tanzania akiwa kazini.
4.0
Adidu za Rejea
Timu
ya uchunguzi iliongozwa na Adidu za Rejea zifuatazo:
4.1
Lengo Kuu
Kuchunguza
hali iliyopelekea kuuawa kwa David Mwangosi.
4.2
Malengo mahsusi
Kuchunguza
chanzo cha kuwepo uhusiano usio mzuri kati ya IPC na uongozi
wa kiutawala wa Iringa .
Kuwahoji
wanakijiji wa Nyololo kuhusu hali halisi iliyosababisha mapambano
kati ya polisi/ Chadema/ waandishi wa habari.
Kukusanya
maelezo stahili kutoka kwa wananchi, IPC na mashuhuda waandishi
waliokuwepo kwenye eneo la ghasia.
Kuchambua
kwa uhuru ripoti za vyombo vya habari, ripoti rasmi na za polisi na madai
kuhusu tukio hilo.
5.0
Muda wa kukamilisha jukumu
Kazi
hiyo ilichukua siku nane (8) kuanzia Septemba 5, 2012 na kumalizika Septemba
12, 2012.
6.0
Methodolojia
Timu
ilianza uchunguzi kama ifuatavyo:
Kwanza
kabisa, hati na taarifa za magazeti kuhusiana na uchunguzi huo zilipitiwa ili
kupata msingi wa suala hilo. Hii inajumuisha mamlaka ya kikatiba ya MCT kufanya
uchunguzi kama huo.
Pili,
Timu hiyo imechunguza kwa karibu jinsi vyombo vya habari vilivyotangaza
zikiwemo picha mgando, na video kuhusu kuuawa kwa Daudi Mwangosi hapo Septemba
2, 2012, na taarifa za awali za polisi dhidi ya mambo yaliyogunduliwa na
wachunguzi katika uchunguzi wao. Taarifa zote zilizoripotiwa na polisi na
Waziri mwenye dhamana kuhusu mauaji ya mwandishi kabla yataarifa ya kuundwa kwa
kamati maalum ya uchunguzi ya Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi
Septemba 4, 2012 yanachambuliwa kwa kina.
Hatimaye,
uchunguzi katika eneo. Hii ilihusisha kusafiri kwenda Iringa na kufanya
mahojiano na watu walioteuliwa na wanahabari katika kijiji cha Nyololo
waliokuwepo siku Mwangosi. Utaratibu wa mahojiano ya mtiririko kutokana na
majibu ulitumiwa na wachunguzi kwa watu mbalimbali.
Utaratibu
mkuu ulikuwa ni mazungumzo ya bayana kati ya wachunguzi na watu mbalimbali
wakiwemo baadhi ya wanakijiji wa Nyololo. Mbinu za kiuchunguzi za uandishi wa
habari zilitumika kufanikisha lengo la jukumu hilo.Matokeo yake, mchakato huo
uliwezesha kupatikana ukweli uliowezesha
kukamilisha ripoti.
7.0
Matokeo
7.1
Maelezo ya awali
Hapo
Septemba 2, 2012, mikutano miwili tofauti ya waandishi wa habari iliyosheheni
ilifanyika katika Manispaa ya Iringa kwa nyakati tofauti siku hiyo. Mkutano wa
kwanza uliitishwa na kuhutubiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC),
Michael Kamuhanda katika ofisi yake asubuhi.
Mada
ya mkutano huo ni uamuzi wa polisi kuzuia mikutano ya kisiasa iliyopangwa na
chama cha upinzani cha Chadema katika mkoa wa Iringa iliyolenga kutelekeza
kampeni za chama hicho za Kuleta Mabadiliko nchi nzima.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa alitahadharisha kuwa sensa ya watu na
makazi
ambayo awali ilikuwa ilipangwa kufanyika Agosti 26 – Septemba 1, 2012,
imeongezewa muda na serikali hadi Septemba 8, 2012, na mikusanyiko ya kijamii
na mikutano ya kisiasa imesimamisha mpaka zoezi hilo likamilike.
Waandishi
wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo wanakiri kwamba katika mkutano huo
marehemu Daudi Mwangosi alikuwa ni ripota pekee aliyemuuliza RPC “maswali
magumu” kiasi cha kumkera kiongozi huyo wa polisi.
Mojawapo
ya maswali yaliyoulizwa na Mwangosi ni ufafanuzi sahihi wa nini hasa ni “
mkutano wa ndani wa chama” kulingana na madai ya maofisa wa Chadema kwamba
chama hicho hakipangi kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa bali
ni kufungua matawi mkoani Iringa bila kufanya mikutano.
Katibu
wa IPC anakumbuka swali moja la Mwangosi kwenye mkutano huo ambalo lilimuudhi
RPC. Aliuliza: kwanini chama tawala cha CCM kiko huru kufanya mikutano ya
kisiasa wakati chama cha upinzani kama Chadema kinawekewa vikwazo na polisi
kila wakati.
Wakati
marehemu Mwangosi akisisitiza ufafanuzi zaidi kutoka kwa Mkuu huyo wa polisi wa
mkoa, RPC alisisitiza : “ Hii ni amri na polisi hairuhusu maswali zaidi kuhusu
suala hili”.
Na
taarifa kutoka kwa RPC imewakumbusha wazi wanasisasa, vyama vya siasa na
wananchi kwa jumla kwamba “mikutano ya vyama vya kisiasa imezuiliwa kutokana na
kuendelea kwa sensa ya watu na makazi kwa siku saba zaidi kuanzia Septemba 2,
2012.
Mara
baada ya mkutano na RPC baadhi ya maofisa wa polisi walionyesha kuwa mambo
hayatakuwa sawa katika kijiji cha Nyololo village Waandishi wengine wa Iringa,
Clement Sanga anayeandikia magazeti ya Mwananchi Communications Ltd na Oliver
Motto, mwandishi wa kujitegemea wa gazeti la Mtanzania, Star TV na Radio Free
Africa walisema haya :
“Baada
ya mkutano huo na waandishi , wakati wanahabari wakitoka kwenye
ofisi za mkoa za Polisi, baadhi ya polisi walisikika bila wao kuwa wakiwaonya
wasiende Nyololo kwa ajili ya kukusanya habari za shughuli za siasa za Chadema
kutokana na kuwa na uwezekano wa hatari”.
Mkutano
wa pili wa waandishi uliitishwa mchana na Chadema na ukahutubiwa
na Katibu Mkuu na Dk.Wilbroad Slaa na kamanda wa Kampeni
ya Mabadiliko ya chama hicho Benson Kigaila.
Katika
mkutano huo , Chadema ilichachamaa na kutetea kampeni zake za mabadiliko na
kushutumu polisi kwa kufanya njama za kuzima kampeni hizo. Chadema ilihoji
kwanini polisi inabagua vyama vya upinzani wakati wakipendelea chama tawala CCM
kwa madai ya kusimamia sheria.
Licha
ya kuwepo amri ya polisi ya kuzuia mikutano yote ya siasa mpaka zoezi la sensa
ya watu na makazi lililoongezewa muda limalizike , Chadema ilidai kwenye
mkutano huo kwamba kampeni za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo
ziliruhusiwa kufanyika katika jimbo la Bububu , Zanzibar.
Kampeni
za uchaguzi mdogo wa Bububu zilizinduliwa Jumapili Septemba 2, 2012 na Makamu
wa Rais wa serikali ya Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Hivyo
kwa ufupi, Chadema iliamua kuendelea na kampeni zake mkoani Iringa , ikiwemo
kufungua matawi ya chama katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi Jumapili
Septemba 2, 2012, lakini bila kufanya mikutano ya hadhara.
Hatimaye
maofisa walishikilia msimamo wao na kuendelea kufufungua matawi ya chama
Nyololo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa Iringa, RPC Michael Kamuhanda, alipanga
askari wake kwenye magari ya wazi kufuatilia msafara wa maofisa wa Chadema.
Pande hizo mbili zilikutana kwenye kijiji cha Nyololo.
Viongozi
wa Chadema walipanga kufungua matawi mawili katika kijiji cha Nyololo village,
kiasi cha kilomita 500 (315 maili) magharibi mwa Dar es Salaam, na mwendo wa
saa tatu kwa gari kutoka Manispaa ya Iringa.
Matawi
hayo yako umbali wa kilomita tatu kutoka kila moja yakitenganishwa
na barabara kuu ya Dar es Salaam -Tunduma.
Mchoro
uliopo ukurasa wa 16 unaonyesha hali halisi ilivyokuwa, kama ilivyoelezwa
na mashuhuda waliokuwepo na kuboreshwa na wachuguzi.
Kwa
lengo la kuonyesha , maeneo mawili yamewekewa alama tofauti ya A ikimaanisha
“eneo tulivu” na B ikimaanisha “eneo la umwagaji damu”.
Katika
eneo la [A], ambapo utulivu ulikuwepo na ulizingatiwa na polisi katika
maamuzi na matendo yao ambapo vurugu na umwagaji damu uliepukwa. Eneo lingine
ni [B], ambapo polisi ilitumia, nguvu zaidi na kupelekea mauaji ya Daudi
Mwangosi na kujeruhi waandishi wengine kadhaa wa Iringa na makada wa Chadema.
7.2
Eneo la matukio ya utulivu [A]
Hapa
ni sehemu ya kwanza lilipo tawi la Chadema kusini mashariki mwa barabara ya
changarawe inayopita kijiji cha Nyololo, kutoka barabara kuu ya Dar-Tunduma.
Mashuhuda
(waandishi na wanakijiji) wal;isema kuwa baada ua kuwasili kwenye eneo la tawi,
maofisa wa Chadema na wanachama walishuka kutoka kwenye magari wakiwa tayari
kuanza shughuli. Ukanda wa njano uliwekwa kuzunguka ofisi ya Chadema kuzuia
watu kukusanyika katika jingo la ofisi hiyo.
Mara
baada ya Chadema kuanza mkutano wao wa ndani kikundi cha askari wa kikosi cha
kuzuia fufo (FFU) kilifika eneo hilo na kujipanga kwa muundo wa kijeshi wa V.
Kikosi hicho kilikua chini ya uongozi wa Ofisa wa kudhibiti uhalifu wa mkoa
(RCO) SSP Nyigesa Wankyo.
Kamanda
wa kikundi cha FFU OC Florent Mnunka anaamuru polisi wainue bendera nyekundu
yenye maandishi ya kuwataka watu waliokusanyika kutawanyika ama vinginevyo
watatumia nguvu. Kamanda huyo anatangaza “Watu wote mliokusanyika hapa,
mnaamriwa na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mtawanyike mara moja na kwa amani,
vinginevyo tutatumia nguvu ” anarudia maneno hayo . Baada ya kurudia amri hiyo
mara tatu, OC-CID anaamuru polisi kusogea karibu na ofisi ya Chadema.
Wakati
wakisogelea eneo hilo la Utulivu [A] , Kamanda wa kampeni ya mabadiliko
ya Chadema Benson Kigaila na viongozi wengine walitoka nje ya ofisi hiyo na
kumuomba kamanda wa FFU kuzuia askari wake kutumia nguvu bila sababu kwa kuwa
haikupanga kufanya mkutano wa hadhara wa kisiasa.
Viongozi
wengine waliokuwa na Kigaila walikuwa ni Alfred Lwakatare na Naibu Katubu Mkuu
wa Chadema Zanzibar , Said Issa Mohamed.
Pande
hizo mbili zilipingana kwa muda kuhusu maana sahihi ya“ mkutano wa ndani wa
chama” na kama maana yake ni tofauti na mikutano iliyozuiwa na polisi .
Ushahidi
wa picha za video uliopatikana na waandishi wa habari wengi unadhihirisha na
kuonyesha mvutano kati ya polisi na Chadema katika eneo tulivu[A] kama
ifuatavyo:
Benson
Kigaila: “ Sisi tuko katika ofisi ya tawi
letu, tunajua sheria , hili ni tawi
la Chadema”.
Kamanda
wa FFU : “Tunawaonyeni nyingi, tafadhali,
fanyeni mkutano
wenu
ndani ya ofisi”
Benson
Kigaila: “Hatuendi kokote ”
Kamanda
wa FFU: “Ingieni ndani”
Ghafla
RCO akaingilia na kushauri viongozi wa Chadema kuwaambia wananchama
wao waingie ndani ya ofisi yao..Wanachama walikubali lakini wote wasingeweza
kutosha kwa sababu ofisi yenyewe ni ndogo. .
RCO
akasisitiza: “Huu ni mkutano usioruhusiwa, tafadhali ingieni ndani”
Mwenyekiti
wa Taifa wa vijana wa Chadema (Bavita), John Heche akajibu :
“Tatizo
ni nini? Kama mmetumwa kuua, fyatueni risasi na muue…sisi tutakaa
hapa.”
Kijana
mmoja wa Chadema anasikika katika video akiwaambia polisi; “Jana
makada wa CCM walirejesha fomu za uchaguzi wa chama chao kwa maandamano na
sherehe … sisi hatuko tayari kuondoka ”.
John
Heche anabishana na polisi akisema : “Mfahamu sheria zenu kabla ya kufanya kazi
yenu”
Mwishowe,
maelewano yalifikiwa kati ya RCO na maofisa wa Chadema, na kamanda anaamuru
maofisa wake kutotumia nguvu dhidi ya watu waliokusanyika kwenye ofisi ile.
Ofisa
mmoja wa Polisi analalamika, “Wanatupotezea muda wetu ….aaah wanachukua muda
wetu”.
Ofisa
huyo inaelekea alikuwa akilalamikia amri ya mwisho iliyotolewa na mkuu wake,
RCO, ikikitaka kikisi hicho kuacha kutumia nguvu, ikiwa inakiuka amri awa
awali.
Waandishi
dhidi ya RPC Kamuhanda
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda anawasili kwenye eneo la utulivu [A]
dakika chake baada ya RCO, maofisa wa FFU na wa Chadema kufikia muafaka na
kukubaliana kuhusu maana ya “mkutano wa ndani”. Waandishi waliokuwepo eneo hilo
walimpokea kwa maswali kadhaa kuhusu tofauti za polisi na Chadema. Marehemu
Daudi Mwangosi akiwa mmoja wa waandishi hao waliomkabili RPC.
Mwangosi
alimuuliza RPC: “Watu hawa wako
katika eneo la ofisi yao, kuna tatizo lolote linalotokana na shughuli
wanazokusudia kufanya?”
RPC
anamjibu Mwangosi “Nimeshakuambia usiwe mbishi.
Nilichokuambia ni kwamba nimezuia mikutano yote ya kisiasa…Lakini usije na
mambo yale yale asubuhi, jioni na mchana, na jua linapozama…kuna umuhimu gani kutuuliza
sisi tupo hapa kufanya nini?”.
Mwandishi
mwingine (Jina lake halikutapitkana )
“Nafikiri wewe ndiye mbishi (RPC)”
RPC
“Nilichozuia ni mikutano ya hadhara
ya kisiasa, lakini shughuli zote za ndani zinaruhusiwa kuendelea…hadi sasa
hakuna tatizo”
RPC
anaendelea: “Tumefanikiwa kuzuia mikutano na
ghasia… kama wanataka
kufanya mikutano ya ndani wanaweza kuendelea.”
Mwangosi
“…kama wanavyofanya sasa …..…”
RPC
anajibu, “Kama walivyofanya tangu juzi ”
Baada
ya kubadilishana maneno zaidi RPC anasema: “Tunawataka
viongozi,
hatutashughulika na watu waliokusanyika hapa. Lengo letu ni kushughulikia
walioitisha mkutano… wao ndio chanzo cha kila kitu, na wanavunja amri rasmi”.
Tunaogopa kuwajeruhi watu bila sababu, hivyo tutashughulika na viongozi ambao
ni kundi dogo na ni rahisi kulishughulikia”
anasema RPC na kuamuru “Sasa hakuna mkutano, huu (mkusanyiko) unaofanyika nje.”
Mwangosi
anaingilia: “ Huu ni mkutano ?
RPC
anaamuru mkusanyiko kuendelea na
mkutano wao ndani; “Ingia ndani”
Mwandishi
(anayetambulika kwa kubeba kamera
na akiwa katika kundi la waandishi): “Inakuwaje kama chumba ni kidogo kutosha
watu wote?”
RPC:
“Tutawakamata ninyi viongozi kama
mtaendelea ”
Sauti
ya mtu anayedhaniwa kuwa kiongozi wa Chadema inasema:
“Tutaendelea
kuwapo hapa .”
RPC:
“Ndiyo na ninyi mko wachache,
tunawamudu ”
Mtu
huyo anajibu : “Aah! Hamna tatizo… ni miaka mingapi
Mandela alikaa gerezani ”?
RPC
anajibu , “ Hata miaka 30, lakini umemtaja
Mandela, wewe Mandela?”
Wakati
waandishi wakimhoji RPC, maofisa wa Chadema waliendelea na mkutano wao na
kuumaliza kwa amani. Chadema walimaliza shughuli yao na wanahabari wakafanya
kazi yao hapa bila kunyanyaswa.
Baaada
ya hapo makada wa Chadema walipanda basi lao kwenda kaskazini magharibi kwenye
ofisi nyingine. Katika eneo hili la utulivu. [A], mabomu ya machozi
hayakulipuliwa wala risasi hazikupigwa kuwatisha watu. Pia hakuna mtu
aliyeuawa.
7.3
Eneo la umwagaji damu [B]
Mara
baada ya maofisa wa Chadema kumaliza ufunguzi wa tawi katika eneo la utulivu
[A], walikwenda kukamilisha shughuli katika eneo la umwagaji damu [B].
Inachukua
chini ya dakika 20 kutembea kufika katika ofisi ya pili ya Chadema.
wakati maofisa wa chama wakielekea katika eneo hilo, polisi waliwafuata kwa
karibu. Waandishi wa habari pia waliwafuatilia ili kukusanya habari za shughuli
hiyo.
Lakini
kitu kimoja kibaya kilitokea hata kabla ya askari wote wa FFU kufika
katika eneo la Umwagaji damu [B].
Mashuhuda
wanaeleza kuwa RPC alimwita RCO na kumuonya wazi kuhusu
“kushughulikia kwa amani’ masuala ya Chadema katika eneo la awali la utulivu [A].
Inaelekea
RCO alijitoa kuelekea eneo la umwagaji damu [B], na hivyo usimamizi wa
utoaji maamuzi katika Eneo la Umwagaji damu [B] ulibakia kwa mkuu wake
ambaye ni RPC Michael Kamuhanda.
Mabishano
na waandishi wa habari kama yaliyotokea katika eneo la la awali yaliibuka tena.
Hapa
makada wa Chadema walikusanyika nje ya ofisi yao wakiimba “Wamezoea
kuua , wamezoea kuua”. Inaelekea wimbo huo uliwaudhi polisi.
Vurugu
zikaanza pale RPC alipoamuru kukamatwa kwa viongozi wa Chadema
waliokuwepo, kwa mujibu wa watu walioshughudia. Kufuataia amri hiyo ya RPC
kulingana na mashuhuda , polisi kwanza waliingia kwa nguvu katika ofisi ya
Chadema, wakipiga mabomu ya machozi na kuaamuru
viongozi hao wajisalimishe.
Baada
ya polisi kutumia nguvu, kiongozi wa kampenu za mabadiliko wa Chadema mkoani
Iringa, Benson Kigaila , aliwaomba wafuasi wachache wa chama hicho na viongozi
waliokuwepo kujisalimisha kwa kuketi na kuinua mikono yao juu”.
Waandishi
wawili waliohojiwa, Clement Sanga wa Mwananchi
Communications
Ltd na Oliver Motto, mwandishi wa kujitegemea wa Mtanzania,
Star TV na Radio Free Africa walishuhudia ghasia hizo katika kijiji cha Nyololo
village, wakati wakiwa wamekimbilia sehemu ya barabarani, hatua chache kutoka
eneo hilo la umwagaji damu B.
Waandishi
hao walisema kuwa wakati makada wa Chadema walitii maagizo
ya viongozi wao ya kuketi na kuinua mikono yao juu, polisi walifyatua
risasi na n a mabomu ya machozi, na kuwapiga makada hao na waandishi kwa
virungu.
7.4
Matukio yasiyo ya kawaida katika Eneo la Umwagaji Damu (B)
Jambo
moja la kushangaza katika eneo la umwagaji damu B ni kuwepo kwa raia
wachache (makada wa Chadema na waandishi kwa pamoja), wakiwa wamezidiwa kabisa
na idadi ya polisi. Maelezo ya mashuhuda, picha mgando na video zinadhihirisha
hii bila shaka yoyote.
Wanakijiji
wa Nyololo waliohojiwa walisema kwamba Jumamosi Septemba
1, 2012 watu wanaoaminika kuwa ni askari kanzu walifika eneo hilo na kuwaonya
wakazi wake kuhusu ya hatari inayowza kutokea kama wakihudhuria shughuli za
ufgunguzi wa matawi ya Chadema. Walidai kuwa walishauriwa pia kuondoka katika
maeneo yao wakati wa saa za mchana Jumapili Septemba 2, 2012 wakati ambao
Chadema imepanga kuendesha shughuli zake.
Mkakati
wa kutisha ulifanikiwa kwa sababu watu wazima wakazi wa Nyololo
waliohojiwa baadaye walisema hawajui kuhusu vurugu za polisi na Chadema kwa
sababu walitelekeza ushauri wa kuondoka katika maeneo hayo.
Mwanamke
mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema:: “Nimejua kuhusu ghasia hizo
na kifo cha mwandishi wa habari kijijini kwetu baada ya kurejea nyumbani
jioni.” Kutokana na uvumi wa vitisho uliosambazwa Jumamosi Septemba 1st, 2012, nilipanga kumtembelea jamaa
yangu aliye mbali kama njia ya kuepuka”.
7.5
Mauaji ya David Mwangosi
Baada
ya kumaliza ukusanyaji wa habari kwa amani katika enelo la utulivu [A], waandishi
wa habari walikwenda katika eneo ambalo liligeuka kuwa mtego wa kifo Eneo la
Umwagaji damu [B] kutoka mwelekeo wa kusini mashariki kupita barabara kuu
ya Dar-Tunduma kumalizia kazia yao.
Alipoangalia
nyuma , Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga
mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe, wa Iringa, Godfrey
Mushi
(32).
Mwandisi
huyo alipigwa mpaka akapoteza fahamu na akapata fahamu akiwa kwenye kituo cha
polisi cha Mafinga. Kamera yake, daftari lake na kalamu havikupatiakana.
Wakati
mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi, marehemu
Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa
mwandishi tu.
Polisi
hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa
amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukiwa Daudi Mwangosi
mwenyewe, kwa vurugu na mabomu ya machozi, na kwanza akapoteza fahamu.
Baada
ya kuona hivyo, Addallah Said mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akamkimbilia
RPC ambaye alikuwa katika gari lake la polisi aina ya Land Cruiser kumuomba
awaamuru askari waache kumpiga mwandishi Daudi Mwangosi.
Wakati
huo huo, inaelekea kutokana na kushangazwa na polisi kumpiga kinyama Daudi
Mwangosi, Mkuu wa polisi wa Mafinga OCD Asseri Mwampamba, aliamua kuingilia ,
kwanza kwa kuwaamuru na kuwaomba askari waache kumpiga marehemu Mwangosi.
Mwandisi
wa ITV, Renatus Mutabuzi ambaye alirekodi tukio hilo “laivu” alithibitisha kwa
timu ya wachunguzi kuwa licha ya jitihada za OCD Asseri kuingilia na kumlinda
Mwangosi kutokana na kipigo, polisi hao hawakumsikiliza.
Wakati
polisi wakiendelea kumpiga Mwangosi, alijaribu kujiokoa kwa kumkumbatia OCD
Asseri Mwampamba, na baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi.
Baadhi
ya waandishi wa Iringa waliokuwa wamejificha waliweza kupiga picha za mgando na
pia za video za vurugu hizo. Waandishi kutoka Dar es Salaam waliweza kukusanya
habari za vurugu hizo kwa sababu tofauti na wenzao wa Iringa, polisi
hawakuwalenga.
Mwanamke
ambaye alijeruhiwa katika vurugu hizo, aliyekuwepo kwenye eneo hilo la
umwangaji damu B alisema kuwa alilala karibu na sehemu ambapo Daudi
Mwangosi aliuawa ili kuepuka kipigo zaidi kutoka kwa FFU. Alizungumza na timu
ya uchunguzi kwa sharti la kutotajawa.
Mwanamke
huyo anadai kuwa aliangalia na hata alimsikia mwandishi Addallah Said
akikikimbilia gari la RPC na kumuomba awaamuru askari wasiendelea kumpiga Daudi
Mwangosi. Alijeruhiwa vibaya na alilazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mafinga
kwa siku tatu.
RPC
hakutekeleza ombi la mwandishi huyo. Badala yake alifunga kioo cha gari lake .
Sekunde chache baadaye gari lake lilipiga honi na wakati huo huo mlipuko wa
bomu la machozi ukasikika na kumua mara moja Daudi Mwangosi.
Kwa
sababu marehemu Mwangosi alikuwa bado chini ya miguu ya OCD Asseri Mwampamba,
naye pia alijeruhiwa katika mlipuko huo.
Picha
za mgando zinaonyesha polisi akipiga bomu la machozi tumboni mwa Daudi kwa
karibu kabisa.
Kwa
masikito makubwa, mwanamke huyo anasema alijua kabisa Daudi Mwangosi ameuawa
mbele ya RPC Michael Kamuhanda.
Kwa
Addallah Said na yule mwanamke , kupigwa kwa honi na kutokea kwa mlipuko kwa
wakati mmoja bado ni kitendawili.
Kwa
kutoamini kilichotokea, , OCD Asseri Mwampamba alilalama kwa uchungu kutokana
na mlipuko wa bomu la machozi akisema: “Sasa, umefanya nini ”?
7.6
Taarifa rasmi zinazokinzana
Taarifa
rasmi lakini zinazokinzana za polisi kuhusu kuuawa kwa David Mwangosi
zilipatikana kwa vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Septemba 3, 2012. Mamlaka
rasmi hazijafuta taarifa hizo mpaka wakati wa kuchapisha taarifa hii.
7.4
Matukio yasiyo ya kawaida katika Eneo la Umwagaji Damu (B)
Jambo
moja la kushangaza katika eneo la umwagaji damu B ni kuwepo kwa raia
wachache (makada wa Chadema na waandishi kwa pamoja), wakiwa wamezidiwa kabisa
na idadi ya polisi. Maelezo ya mashuhuda, picha mgando na video zinadhihirisha
hii bila shaka yoyote.
Wanakijiji
wa Nyololo waliohojiwa walisema kwamba Jumamosi Septemba
1, 2012 watu wanaoaminika kuwa ni askari kanzu walifika eneo hilo na kuwaonya
wakazi wake kuhusu ya hatari inayowza kutokea kama wakihudhuria shughuli za
ufgunguzi wa matawi ya Chadema. Walidai kuwa walishauriwa pia kuondoka katika
maeneo yao wakati wa saa za mchana Jumapili Septemba 2, 2012 wakati ambao
Chadema imepanga kuendesha shughuli zake.
Mkakati
wa kutisha ulifanikiwa kwa sababu watu wazima wakazi wa Nyololo
waliohojiwa baadaye walisema hawajui kuhusu vurugu za polisi na Chadema kwa
sababu walitelekeza ushauri wa kuondoka katika maeneo hayo.
Mwanamke
mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema:: “Nimejua kuhusu ghasia hizo
na kifo cha mwandishi wa habari kijijini kwetu baada ya kurejea nyumbani
jioni.” Kutokana na uvumi wa vitisho uliosambazwa Jumamosi Septemba 1st, 2012, nilipanga kumtembelea jamaa
yangu aliye mbali kama njia ya kuepuka”.
7.5
Mauaji ya David Mwangosi
Baada
ya kumaliza ukusanyaji wa habari kwa amani katika enelo la utulivu [A], waandishi
wa habari walikwenda katika eneo ambalo liligeuka kuwa mtego wa kifo Eneo la
Umwagaji damu [B] kutoka mwelekeo wa kusini mashariki kupita barabara kuu
ya Dar-Tunduma kumalizia kazia yao.
Alipoangalia
nyuma , Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga
mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe, wa Iringa, Godfrey
Mushi
(32).
Mwandisi
huyo alipigwa mpaka akapoteza fahamu na akapata fahamu akiwa kwenye kituo cha
polisi cha Mafinga. Kamera yake, daftari lake na kalamu havikupatiakana.
Wakati
mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi,
marehemu
Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa
mwandishi tu.
Polisi
hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa
amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukiwa Daudi Mwangosi
mwenyewe, kwa vurugu na mabmu ya machozi, na kwanza akapoteza fahamu.
Baada
ya kuona hivyo, Addallah Said mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akamkimbilia
RPC ambaye alikuwa katika gari lake la polisi aina ya Land Cruiser kumuomba
awaamuru askari waache kumpiga mwandishi Daudi Mwangosi.
Wakati
huo huo, inaelekea kutokana na kushangazwa na polisi kumpiga kinyama Daudi
Mwangosi, Mkuu wa polisi wa Mafinga OCD Asseri Mwampamba, aliamua kuingilia ,
kwanza kwa kuwaamuru na kuwaomba askari waache kumpiga marehemu Mwangosi.
Mwandisi
wa ITV, Renatus Mutabuzi ambaye alirekodi tukio hilo “laivu” alithibitisha kwa
timu ya wachunguzi kuwa licha ya jitihada za OCD Asseri kuingilia na kumlinda
Mwangosi kutokana na kipigo, polisi hao hawakumsikiliza.
Wakati
polisi wakiendelea kumpiga Mwangosi, alijaribu kujiokoa kwa kumkumbatia OCD
Asseri Mwampamba, na baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi.
Baadhi
ya waandishi wa Iringa waliokuwa wamejificha waliweza kupiga picha za mgando na
pia za video za vurugu hizo. Waandishi kutoka Dar es Salaam waliweza kukusanya
habari za vurugu hizo kwa sababu tofauti na wenzao wa Iringa, polisi
hawakuwalenga.
Mwanamke
ambaye alijeruhiwa katika vurugu hizo, aliyekuwepo kwenye eneo hilo la
umwangaji damu B alisema kuwa alilala karibu na sehemu ambapo Daudi
Mwangosi aliuawa ili kuepuka kipigo zaidi kutoka kwa FFU. Alizungumza na timu
ya uchunguzi kwa sharti la kutotajawa.
Mwanamke
huyo anadai kuwa aliangalia na hata alimsikia mwandishi Addallah Said akikikimbilia
gari la RPC na kumuomba awaamuru askari wasiendelea kumpiga Daudi Mwangosi.
Alijeruhiwa vibaya na alilazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mafinga kwa siku
tatu.
RPC
hakutekeleza ombi la mwandishi huyo. Badala yake alifunga kioo cha gari lake .
Sekunde chache baadaye gari lake lilipiga honi na wakati huo huo mlipuko wa
bomu la machozi ukasikika na kumua mara moja Daudi Mwangosi.
Kwa
sababu marehemu Mwangosi alikuwa bado chini ya miguu ya OCD Asseri Mwampamba,
naye pia alijeruhiwa katika mlipuko huo.
Picha
za mgando zinaonyesha polisi akipiga bomu la machozi tumboni mwa Daudi kwa
karibu kabisa.
Kwa
masikito makubwa, mwanamke huyo anasema alijua kabisa Daudi Mwangosi ameuawa
mbele ya RPC Michael Kamuhanda.
Kwa
Addallah Said na yule mwanamke , kupigwa kwa honi na kutokea kwa mlipuko kwa
wakati mmoja bado ni kitendawili.
Kwa
kutoamini kilichotokea, , OCD Asseri Mwampamba alilalama kwa uchungu kutokana
na mlipuko wa bomu la machozi akisema: “Sasa, umefanya nini ”?
7.6
Taarifa rasmi zinazokinzana
Taarifa
rasmi lakini zinazokinzana za polisi kuhusu kuuawa kwa David Mwangosi
zilipatikana kwa vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Septemba 3, 2012. Mamlaka
rasmi hazijafuta taarifa hizo mpaka wakati wa kuchapisha taarifa hii.
7.7
Taarifa rasmi katika muktadha
Kwa
upande mmoja Waziri wa Mambo ya Ndani anakiri 4/09/2012 kwamba
Daudi Mwangosi aliuawa na bomu la machozi ambalo halikuwa limeshughulikiwa
vizuri, siku inayofuata RPC wa Iringa anatokea kwenye televisheni akitangaza
habari za kuwatupia lawama wafuasi wa Chadema kwa kutupa kitu kizito
kilicholipuka na kumuua Mwanjisi, kujeruhi watu kadhaa wakiwemo maofisa wa
Polisi.
Mashuhuda
na mambo kadhaa yaliyochukuliwa kwa video na picha mgando
zinaonyesha kuwa hakukuwa na kundi la watu bali ni wanahabari na baadhi ya viongozi
wa Chadema ambao walikuwa wachache kulinganisha na idadi ya polisi. Hata hivyo
RPC anadai kuwa kuiikuwa na kundi la watu wakifanya vurugu.
Pia
polisi na taarifa zingine rasmi zimeacha kueleza kuwa tukio la ufunguzi
wa tawi lilifanyika katika eneo tulivu A bila ghasia.
Septemba
12, 2012 Konstebo wa Polisi, Cleophase Pasifious Simon (23) alifikishwa
mahakamani kwa akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi.
.Ushahidi
unaonyesha kuwa marehemu Mwangosi alikuwa amezingirwa na akipigwa na polisi
wasiopungua saba. Polisi mmoja akiwa amelenga bunduki la kupigia bomu la
machozi tumboni mwa Mwangosi.
Kukamatwa
kwa Konstebo wa polisi na kushitakiwa kunathibitisha Waziri wa Mambo ya Ndani
alichomwambia Katibu Mtendaji wa MCT kuhusu bomu la machozi “kutokushughulikiwa
vizuri” kinyume na jitihada za kuficha ukweli za RPC wa Iringa, Michael
Kamuhanda na maofisa wa polisi wa makao makuu ya polisi mjini Dar es Salaam.
Cha
kushangaza, wakati akihutubia mkutano wa wanahabari uliovunjika mjini Iringa
Septemba 5, 2012 , Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai, (DCI), Robert
Manumba alisema “matukio ya aina hii yapo na yataendelea kutokea”. Matamshi
haya yalitangazwa sana na vyombo vya habari. Manumba alikuwa akijaribu kuwasihi
wanahabari wa Iringa ambao waligomea mkutano aliouitisha mpaka maofisa wote wa
polisi wa Iringa waondoke kwenye ukumbi waliokuwemo. Mgomo huu ulichukuliwa kufuatia
uamuzi wa IPC kugomea kuandika habari za polisi mkoani humo mpaka uchunguzi
kuhusu kuuawa ukamilike Daudi Mwangosi.
8.0
Iliyobaki yote ni historia
Kilichowashangaza
waandishi katika hatua hii ni kwamba ghafla polisi waliwageuka. Hata baada ya
kuona kuwa mambo yamekuwa mabaya na kukimbia kujifisha kwenye vichaka vya
karibu, polisi waliwafuata na kuwalenga kwa mabomu ya machozi huku wakikimbia.
Francis
Godwin, mwandishi wa kujitegema, shuhuda na Naibu Katibu Mkuu
wa IPC anakumbuka kuwa polisi wawili walimfukuza mpaka kwenye
vichaka vya kijiji cha Nyololo ambapo alilazimika kuacha gari lake
na kurejea usiku kulifuata.
Wakiwa
katika sehemu walipojificha, waandishi walikuwa wakimsaidia Abdallah Said
kuondoa vipande vya nyama ya binadamu vilivyompata kutoka katika mwili wa Daudi
Mwangosi.
Baada
ya mkutano wa waandishi wa habari wa asubuhi katika ofisi za RPC, waandishi
waliokuwepo wanakumbuka kuwa askari mmoja mpelelezi alimfuata Mwangosi na
kumwambia : “Ina maana gani kwenda Nyololo kuandika habari za shughuli za
Chadema ambazo zinaweza kuishia na kifo chako”?
Akiwa
anatabasamu, Mwangosi alisema: “nikifa leo, mwili wangu hautazikwa
ardhini lakini katika mioyo ya watu”. Ilikuwa kama vile anatabiri
kifo chake.
Katibu
wa IPC Frank Leonard haelewi kwanini polisi waliwageuka waandishi
wenzake.
“Kila siku saa tano asubuhi ,
tunashiriki katika mkutano wa waandishi wa habari unaoitishwa na RPC ofisini
kwake. Sisi na maofisa wake tunajua sana na hata kwa majina. Ni kitendawili
kikubwa Polisi wamewashambulia waandishi wakiwa kazini na hatimaye kumuua Daudi
Mwangosi”.
Katika
eneo moja [A], kulikuwa na utulivu ambapo vurugu na umwagaji damu
haukuwepo ambapo katika eneo lingine [B], polisi walitumia nguvu ya
ziada, kupelekea kuuawa kwa Daudi Mwangosi na kujeruhiwa makada wengine kadhaa
wa Chadema.
9.0
Shutuma na kulaaniwa kwa hapa nchini na kimataifa
MCT
Baraza
la Habari Tanzania (MCT) limelaani vikali tukio hilo ambalo ni tishio la moja
kwa moja kwa uhuru wa vyombo vya habari. “Hili ni tukio la kwanza kwa mwandishi
wa habari kuuawa akiwa kazini”, Katibu Mtendaji wa alikaririwa na vyombo vingi
vya habari akisema.
MCT
inataka mamlaka husika kufanya kila liwezekanlo kuhakikisha kuwa ukweli wa
kilichotokea katika siku ya mauaji hayo ya kikatili unajulikana.
MCT
imeshutumu kuwahusisha wanahabari na shughuli za kisiasa na kumuhusisha
na chama cha siasa wakati alikuwa akifanya kazi yake UTPC
Taarifa
ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umeshutumu
vikali mauaji ya Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi wakati
akitekeleza kazi zake kama mwandishi wa habari. Taarifa hiyo imeitaka
serikali kuwawajibisha mara moja polisi waliohusika na operesheni iliyopelekea
kifo cha Mwangosi.
UTPC
imetaka kufukuzwa kazi mara moja kwa maofisa waliohusika na kifo marehemu Daudi
Mwangosi.
Jukwaa
la Wahariri Tanzania (TEF)
Jukwaa
la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali mauaji ya Mwangosi mikononi mwa
polisi.
Katibu
Mkuu wa TEF, Neville Meena, anasema hii ni mara ya kwanza katika
historia ya sasa Tanzania kwa mwandishi kuuawa akiwa kazini.
MISA
na wengine
Taasisi
ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika (MISA), Kamati ya Kulinda Waandishi
wa Habari (CPJ) na ARTICLE 19, zote zimelaani kuuawa
kwa Daudi Mwangosi akiwa mikononi mwa polisi.
Levi
Kabwato, ofisa Programu wa MISA anayeshughulikia Ufuatiliaji wa Uhuru wa Vyombo
vya Habari na Utafiti, alieleza katika taarifa kustushwa kwake na mauaji ya
Mwangosi.
“Hii
inastusha. Septemba 2 2012, si siku mbaya kwa uandishi wa habari wa Tanzania
bali kwa eneo zima na dunia yote. Ghasia siyo jibu, hazitatui kitu.
Tunaitaka
serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na kuwawajibisha wote waliohusika na
upotefu wa maisha,” Kabwato alisema katika taarifa.
CPJ
inasema kwamba kifo cha Mwangosi ni cha kwanza kwa mwanahabari aliye kazini
nchini Tanzania tangu taasisi hiyo ilipoanza kuweka rekodi za kina 1992 ARTICLE
19 imeeleza kusikitishwa na mauaji ya Daudi Mwangosi mikononi mwa Polisi wa
Tanzania, na kuitaka serikali ihakikishe wote waliohusika wanashitakiwa.
Unesco
Mkurugenzi
Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, pia alishutumu mauaji ya mwandishi wa habari wa
Tanzania, Daudi Mwangosi Septemba2, 2012 na kuitaka serikali kuchunguza mauaji
hayo.
UNESCO
inataka serikali ichunguze kifo hicho na kuwashitaki wote wanaohusika.
Taarifa
ya UNESCO inasema: “ Ni muhimu kwa demokrasi na utawala wa sheria kwamba
waandishi waruhusiwe kufanyakazi zao na kutumia haki yao ya kujieleza kwa
usalama.”
10.0
Hitimisho na Mapendekezo
Mauaji
ya David Mwangosi mikononi mwa polisi wakati akiwa kazini ni tishio kwa uhuru
wa habari.
Uhuru
wa habari ni kumwezesha waandishi kufanyakazi bila vitisho ama ghasia na waweze
kuripoti wakiwa huru bila kudhibitiwa.
Kama
mwandishi, Daudi Mwangosi alikuwa akitimiza haki yake ya kikatiba
kufanya “kazi nzuri”.
Kwa
vyombo vya habari na hasa waandishi, haijalishi kama Kamanda wa Mkoa wa Polisi
ameipiga marufuku shughuli za Chadema katika kijiji cha Nyalolo au la.
Ilikuwa
ni jambo ka maslahi ya umma kwa vyombo vya habari ambalo vyombo vya habari
vilistahili kuripoti kadri mambo yalivyokuwa yaakiendelea na watu wenyewe
kufanya uamuzi.
Kimsingi,
wakati wote na katika matukio yote, mazuri ama mabaya, waandishi
lazima wawepo na wachukuliwe kama watu wasio na upande wowote.
Pia,
Polisi walitumia nguvu ya ziada bila sababu dhidi ya watu wasio na silaha
katika kijiji cha Nyololo village.Katika hatua ya mwisho, ikawa vita ya polisi
dhidi ya waandishi wa habari na hatimaye kuuawa kwa Daudi Mwangosi.
Timu
ya uchunguzi haikubali kabisa suala la kukosea utambulisho wa mtu.
Waandishi
wanane waliokuwep katika kijiji cha Nyololo waliweza kutambulika
kwa urahisi, hasa kutokana na mambo kwenda salama katika eneo la uslamaa [A].
Waandishi
walikuwa na Kamera, vidaftari na kalamu na wengine kama sio wote walikuwa
wanafahamika sana na polisi wa Iringa.
Sasa
imebainika wazi kwamba Polisi walikuwa wanawawinda waandishi wa Iringa ambao
walikuwa wakiwajua.
Mapambano
ya Chadema na Polisi katika Kijiji cha Nyololo habari zake zilikusanywa na
waandishi kutoka Dar es Salaam pia. Kwanini walikuwa waandishi wa Iringa ndiyo
walilengwa katika ghasia hizo.!
Uhasama
na chuki iliyokuwepo kati ya RPC wa Iringa na marehemu Daudi Mwangosi katika
kipindi chote cha saa kadhaa tangu mkutano wa waandishi wa habaria na dakika
chache kabla ya mauaji yake mbele ya RPC huyo huyo katika kijiji cha Nyololo
Septemba 2, 2012 unaibua maswali mengi kuliko majibu.
Waandishi
sita wa Iringa wameathirika na msongo wa mawazo kutokana na kiwango cha ghasia
walizofanyiwa na polisi na wanafikiria kuachana na kazi ya uandishi. Mmoja
anapanga kuwa mchungaji kwa kuhofia maisha yake.
Mamlaka
husika zahitaji kuwa na mipango ya kuwaelimisha polisi jinsi ya kushughulika na
vyombo vya habari hasa na wandishi wa habari. Lengo liwe kuboresha mahusiano ya
kikao kati ya pande hizo mbili..
Hii
inatokana na uhusiano mbaya iliyoibuka kati ya waandishi wa Iringa na polisi wa
mkoa tgangu robo ya mwisho wa 2011. Uhusiano huu kati ya pande hizi mbili
umekua tangu 2011 ambapo aliyekuwa OCD wa Iringa Mohamed Semunyu alipoamriwa
ana bosi wake kulipa kamera ya mwandishi
aliyoiharibu bila sababu ya maana.
Inashinda
ufahamu wa kawaida kwamba matukio mawili ya yanayofanana katika siku moja
ynashughulikiwa tofauti.: Moja linashughulikiwa na ukatili na nguvu kubwa kwa
kuwalenga wanahabari wa Iringa.
Katika
tukio la kwanza, RCO aliamua Chadema wanaweza kuendelea na masuala yao ya ndani
katika ofisi yao na katika tukio la pili Mkuu wa polisi wa mkoa anaamua
shughuli hizo zisimamishwe kwa vyovyote na hata kwa nguvu.
Akigusia
kwa kiasi mpambano wa Nyololo kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema, Rais Jakaya
Kikwete katika hotba yake ya kila mwezi kwa taifa kwa mwezi wa September 2012,
alisisitiza polisi kuepuka matumizi ya nguvu za kupita kiasi na kuwakumbusha
watanzania na wanasiasa kuheshimu sheria za nchi na kuiona polisi kama
wasimamizi wa amani na usalama.
Rais
alifafanua kuwa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kuruhusu au kuzuia haki ya
kufanya mikutano na maandamano ya vyama vya siasa.
Taarifa
za awali za maofisa wa ngazi za juu kuhusu mauaji ya M wangosi zilitofautiana
na mtu anapoziangalia kutokana na ushahidi uliopatikana ni dhahiri kulikuwa na
jitihada za kuficha ukweli.
Tukio
hilo limeharibu sifa ya Tanzania kimataifa kama nchi ya amani na ya demokrasia.
Mauaji
ya Mwangosi yalitokea wakati wa kufanyika mkutano wa Chama cha Umoja wa
Mabaraza ya Habari Duniani (WAPC) ambapo MCT ilikuwa mwenyeji wake.
Katibu
Mkuu wa WAPC, Chris Conybeare, alimwambia waziri wa Habari, Dk. Fenella
Mukangara: “Wakati waandisi wanauawa demokrasi pia inakufa.. tukio hili moja
limeanza kuichafua sifa yaTanzania ya kuendeleza uhuru wa habari”.
Zaidi
ya Polisi saba chini ya uongozi wa RPC Michael Kamuhanda kwa
pamoja
wamemzingira na kumpiga Daudi Mwangosi. Kwanini wengine hawajashitakiwa, si
suala linalohitaji uelewa wa kawaida.
Hata
hivyo uchunguzi hauwezi kuthibitisha kama mauaji hayo ya Mwangosi yalipangwa.
No comments:
Post a Comment