Nelson (katikati) akiwa na wazazi wa Adam (aliyebebwa).
Kijana jasiri mwenye miaka 16 amehatarisha maisha yake kumwokoa mtoto mdogo aliyenasa ndani ya nyumba iliyokuwa ikiteketea moto.Nelson Fonangwan alikuwa amelala lakini akaingia kazini baada ya kusikia vilio vya kuomba msaada vya jirani na kukuta moshi mweusi ukivuma kutoka kwenye nyumba hiyo iliyoko Southampton, huko Hampshire.
Mama wa watoto wawili Aneta Jedlikoswka, mwenye miaka 32, alikuwa akihangaika kujaribu kutoboa tundu kwenye dirisha jikoni kuweza kumfikia mtoto wake wa kiume mwenye miaka miwili, Adam, ambaye alikuwa akigonga gonga vioo kutokea kwa ndani.
Nelson, mwanafunzi wa Chuo cha Richard Taunton Sixth Form jiji humo, alijitosa ndani ya nyumba hiyo kupitia dirishani wakati mama yake akipiga simu polisi kuomba msaada zaidi, na kutambaa kabla ya kumwokoa mtoto.
Aliliambia Gazeti la Southern Daily Echo: "Siamini ninachokiona. Binti alikuwa akigonga vioo na kutengeneza tundu. Alijikata na alikuwa akichuruzika damu.
"Alikuwa ameumia lakini alichokuwa akifikiria ni mtoto wake. Hazungumzi Kiingereza fasaha na alinyooshea kidole kwangu kuelekea nyumba yake na kusema 'mtoto', nikajua nahitajika kufanya uamuzi mgumu."
Alisema moshi ulikuwa mzito na kukiri alilazimika kuwa mwendawazimu kidogo kabla ya kuingia kwenye nyumba. Pale alipomtoa nje Adam, alisema Aneta alimkumbatia mtoto kwa nguvu na hisia kali.
Kisa kizima kilianza baada ya Aneta kwenda kutupa uchavu nje na kujikuta akifungiwa nje pale mlango ulipojibamiza kwa nguvu. Akiwa bado kakwama nje, jiko lililokuwa limewashwa likashika moto.
Vikosi vya zimamoto, polisi na madaktari walikwenda eneo la tukio. Alipelekwa Hospitali Kuu ya Southampton ambako alifanyiwa upasuaji katika majeraha mawili mkononi mwake.
Aneta aliliambia Gazeti la Southern Daily Echo: "Ilikuwa faraja. Nilifurahi sana kuungana na furaha zaidi ni kwamba hayuko ndani tena. Kuliwa na moshi mwingi na ingeweza kuwa hatari mno. Siwezi kumshukuru kiasi cha kutosha."
Nelson, ambaye asili yake ni kutoka Cameroon, Afrika Magharibi, anasomeaafya na ustawi wa jamii, Hisabati, Kiingereza na Michezo. Mkuu wake wa chuo, Alice Wrighton alisema: "Wote tunasikia fahari kwa kitendo kishujaa alichofanya Nelson."
No comments:
Post a Comment