Msichana wa miaka 17 amefariki baada ya kupoteza kiasi kikubwa cha damu iliyokuwa ikivuja ndani ya mwili baada ya kufanyiwa oparesheni ya kawaida ya kidole-tumbo (appendix).
Victoria Katie Harrison anayeishi Wellingborough, huko Northamptonshire, alilazwa katika Hospitali Kuu ya Kettering kwa ajili ya kuandaliwa utaratibu Agosti 15 mwaka huu.
Kijana, imara na mwenye afya njema, oparesheni ya mpambaji nywele huyo aliye mafunzoni ilitakiwa kuwa ya moja kwa moja. Badala yake, akaanza kutokwa damu kwa kiasi kikubwa mno.
Licha ya majaribio kadhaa bila mafanikio kuokoa maisha yake, Victoria alifariki siku iliyofuata. Uchunguzi kuhusu kifo chake sasa umeanza.
Familia ya Victoria imedai kifo chake kinaweza kuwa kimesababishwa na wapasuaji kwa bahati mbaya kupakata mshipa mkubwa wa damu wakati wakipachika kamera ndogo ya uchunguzi kwenye tumbo lake.
Kidole-tumbo kwa kawaida huondolewa kwa kutoboa tundu dogo na hivyo kumfanya mgonjwa kukaa hospitali kwa muda mfupi na kupona haraka. Inachukua takribani dakika 30 kwa kuwekewa nusukaputi.
Mpasuaji hukata sehemu mbili au tatu ndogo zenye ukubwa wa sentimeta 1 kila moja katika sehemu ya chini ya utumbo na kupenyeza kifaa maalumu ndani kuondoa kiungo hicho.
Kamera ndogo pia huingizwa kumwezesha mpasuaji kuweza kuona kinachoendelea ndani ya mwili wa mgonjwa. Pindi kidole-tumbo kinapoondolewa, matundu hayo madogo huzibwa kwa kushonwa nyuzi ama kuwekwa gundi maalumu.
Mama wa Victoria aliyehuzunishwa, Tracy Foskett ameweka kila kitu kwenye mtandao wa Facebook kattika kumkumbuka binti yake kuelezea kwa marafiki zake kwanini alifariki.
Aliandika: "Ni kutaka kila mmoja afahamu, Victoria alikuwa kutokana na kuvuja damu ndani kwa ndani kutoka katika mpasuko katika tundu ambako kamera ilichomekwa. Lakini hakuugua.
Baadaye aliongeza: "Alikuwa msichana mwenye upendo - kila mmoja walimwita rafiki yao mkubwa. Alikuwa pia rafiki yangu mkubwa. Alipendwa na watu wengi sana na alikuwa maarufu mno.
Zaidi ya watu 300 walihudhuria msiba wa Victoria, ambaye alifahamika kama 'Tor', wakati alipowekwa kwenye nyumba yake ya milele mwezi uliopita.
Alizikwa ndani ya jeneza la rangi ya pinki.

No comments:
Post a Comment