MAUAJI NCHINI SYRIA SASA YAFIKIA PABAYA...


KUSHOTO: Mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya kutokana na milipuko ya mabonu. JUU: Mwili wa msichana mdogo ukiwa umetelekezwa mtaani baada ya shambulio la mabonu. CHINI: Mabaki ya majengo  baada ya mashambulio manne ya mabomu.
Mwili wa msichana mdogo aliyepoteza uhai umelala mtaani, mwathirika asiye na hatia wa mfululizo wa mashambulizi ya mabomu ya kujitoa mhanga ambayo jana yameteketeza katikati ya mji wa Aleppo nchini Syria.
Kijana huyo ambaye amepigwa picha akiwa amelala kwenye mtaa uliotapakaa damu, ni mmoja kati ya takribani waathirika 40 wa milipuko hiyo ya jana asubuhi, ambayo inaweza kuashiria hatua nyingine ya vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika ishara ya kukua kwa chuki ya mgogoro kati ya waasi na vikosi vya askari watiifu kwa Rais Bashar al-Assad, kitovu cha mji huo cha Saadallah al-Jabari Square kilishambuliwa kwa milipuko minne - kama ile ambayo mpaka sasa imeshaelekezwa katika mji mkuu wa Damascus.
Na huku kukiwa na hofu ya kutokea milipuko mingine zaidi, mwili wa msichana huyo mdogo - ishara dhahiri ya madhara zaidi kila upande ukijiandaa kufanya - umeacha ukiwa umetelekezwa katika mtaa huku wananchi wakiwa wamejaa hofu ya kutokea milipuko zaidi.
Wakati huohuo, makombora ya Syria yametua katika mji wa jirani nchini Uturuki, na kuua takribani watu watano, akiwamo mtoto wa kiume mwenye miaka sita.
Abdulhakim Ayhan, Meya wa mji wa Akcakale nchini Uturuki mpakani na Syria, alisema mtoto huyo na mwanamke mmoja walikuwa ni miongoni wa waliokufa kutokana na mashambulio ya mkombora hayo.
Wakazi wa mji huo waliojawa na ghadhabu waliandamana hadi ofisi ya Meya huyo kulaani mauaji hayo.
Wakati huohuo, maofisa wa serikali wamewalaumu 'magaidi' wa waasi kwa kufanya vurugu katika kitovu cha mji wa Aleppo, ambao unatawaliwa na vikosi vya askari wa Rais Assad.
Mlipuko wa tano uliripotiwa mita 100 tu kutoka Bab al-Jinein, karibu na Chama cha Wafanyabiashara na klabu moja ya maofisa. Eneo hilo liko katika ukingo wa Old City, ambako watu wengi wanaikimbia mapigano wamekuwa wakipigana.
Ofisa ambaye hakufahamika alieleza mapema kwamba watu 29 waliuawa na wengine 70 kujeruhiwa katika milipuko hiyo, lakini ripoti za hivi karibuni kutoka upinzani zimesema takribani watu 40 wamekufa na zaidi ya 90 kujeruhiwa.
Kituo cha televisheni ya serikali Syria cha Al-Ikhbariya TV kimeonesha picha za uharibifu makubwa kutoka eneo ilipotokea milipuko hiyo. Imeiita milipuko hiyo kama kazi ya 'magaidi', neno ambalo serikali imekuwa ikilitumia kuwaelezea waasi wanaopigana kumng'oa madarakani Assad.
Kituo hicho kilionesha picha na miili ya wanaume wanne waliouawa, akiwamo mmoja ambaye mwili wake ulitapakaa vumbi ukikokotwa kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoanguka na kupakiwa kwenye gari ya mizigo. Ilielezwa mapema magari mawili yaliyosheheni mabomu yalitumika kwenye shambulio hilo.
Kituo hicho pia kilionesha picha za miili ya wanaume watatu waliokufa waliojifanya ni askari wa jeshi wachovu ambao inasemekana waliuawa na vikosi vya ulinzi kabla ya kulipua mabomu yaliyofungwa kwenye mikata waliyokuwa wamevaa. Mmoja alionekana akiwa ameshikilia mkononi chombo cha kufyatulia risasi.
Katika kipindi chote cha miezi 18 ya harakati za mabadiliko dhidi ya Rais Assad, mashambulio ya kujitoa mhanga na ulipuaji magari yaliyolenga ofisi za usalama na askari vimeshika kasi katika Syria, hasa katika mji mkuu wa Damascus.
Lakini Aleppo imekuwa ikinusurika kutokana na mabomu hayo na kutoka msukosuko ambao uliikumba miji mingine ya Syria, hasa katika mwaka wa kwanza wa uasi huo.
Ndipo, Februari, mashambulio mawili ya kujitoa mhanga kwenye magari ilipiga jengo la usalama katika eneo la viwanda la mjini Aleppo na kuua watu 28.

No comments: