MWANAMUZIKI WYCLEF JEAN ATANGAZA KUMALIZA BIFU NA LAURYN HILL...



Wyclef Jean amesema hana tena chuki na Lauryn Hill ...licha ya kusema dada huyo alimzushia kuzaa naye mtoto wake wa kwanza siku za nyuma.
Jean alikuwa mjini New York juzi ndipo akaulizwa kuhusu ufafanuzi katika kitabu chake kipya "Purpose" ...mojawapo ikiwa ni kukiri kwake kwamba alikuwa na mahusiano na dada huyo mwimbaji wa zamani wa kundi la Fugees.
Katika kitabu hicho, Wyclef aliandika: "Nilifunga ndoa na Lauryn na nilikuwa na mahusiano naye, lakini alinifanya niamini kwamba mtoto huyo alikuwa wangu, na siwezi kusamehe kwa hilo." Kundi hilo likasambaratika muda mfupi baadaye.
Lakini juzi, Wyclef alieleza hajutii kuielezea dunia kuhusu hilo ...lakini anataka watu waelewe hana tena kinyongo na Lauryn.
"Hivi ndivyo ninavyojisikia," Jean alieleza ...akiongeza, "Kwa kipindi hicho, kilikuwa ni kitu nilichokuwanacho ...na ninayo furaha kusema kwamba nimekiondoa kabisa."

No comments: