MKALI WA KIPINDI CHA CBEEBIES ATUPWA JELA...

Michael Offei katika moja ya pozi zake kwenye filamu.
Watoto wa sehemu zote Uingereza wanaifahamu sura yake wakati wakitazama kipindi cha CBeebies, lakini Michael Offei hataweza kuonekana tena kwenye televisheni kwa kipindi kirefu.
Mtu huyo mwenye miaka 46 anatumikia kifungo cha siku 28 jela baada ya kushindwa kulipa Pauni za Uingereza 42,000 kwa ajili ya matunzo ya mtoto wake mwenyewe wa kiume.
Nyota huyo wa televisheni, ambaye anafahamika kama Byron Wandsworth kwenye kipindi cha watoto cha Storymakers, alipewa hukumu hiyo baada ya kutotokea mahakamani mara mbili katika tarehe zilizopangwa kusikilizwa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, hati ya kukamatwa kwake ilitolewa na baadaye kufikishwa mbele ya hakimu.
"Kama angejaribu kulipa chochote, kiasi chochote cha pesa katika miaka michache iliyopita, tungehukumu tofauti," Mwenyekiti Dennis Alderman alimweleza.
Offei si tu kwamba anatokea kwenye kipindi cha CBeebies, lakini pia alicheza kwenye filamu ya James Bond 'Casino Loyale', lakini pia alishirikiana na Dougray Scott katika filamu ya Hitman.
Mashitaka ya Offei katika mahakama ya Enfield yamekuja baada ya Serikali kuidhinisha kutolewa kiasi Pauni za Uingereza milioni 13.5 kutoka kwenye akaunti za benki za wote wanaokwepa kulipa gharama za matunzo ya watoto.
"Wazazi wanaojaribu kukwepa wanachodaiwa wanadanganya watoto wao katika mapato yao taslimu," msemaji wa Idara ya Kazi na Pensheni alieleza.

No comments: