CHEKA TARATIBU...

Mkuu wa Kikosi cha Jeshi kamtuma Kamanda kwenda kumtaarifu mmoja wa askari wake waliokuwa mafunzoni kwamba mama yake amefariki. Kamanda akaitisha paredi na kutangaza, "Askari kumi waende kuchanja kuni na waliobaki wafanye usafi wa mazingira. Halafu kabla sijasahu, Chacha mama yako kafariki!" Mkuu wa Kikosi alipopata taarifa zile akamwita Kamanda wake na kumweleza, "Hukufanya sawa kumweleza Chacha, unatakiwa utumie mbinu na ujanja unapompa mtu taarifa kama hizo." Baada ya miezi kadhaa kupita, zikafika taarifa nyingine kwamba askari anayeitwa Matata kafiwa na baba yake. Kama kawaida Mkuu wa Kikosi akamtuma Kamanda na kumtaka atumie mbinu kufikisha taarifa. Kamanda akaitisha paredi na kusema, "Wote wenye baba wasogee hatua tatu mbele! We Matata baki hapo hapo!" Duh, kasheshe...

No comments: