AMCHAPA VIBAO BIBI KWA KUENDESHA GARI KWA SPIDI NGOGO...

Dereva mgomvi amemzaba kibao bibi kizee usoni baada ya kukasirishwa na uendeshaji wake gari taratibu.
Usman Yasin mwenye miaka 30, alimshambulia bibi huyo mwenye miaka 81 baada ya kufungulia mvua ya matusi kwa bibi huyo kwa kuendesha gari spidi ndogo ya maili 5 kwa saa wakati akielekea kwenye nyumba ya kutunzia wazee kumtembelea mumewe.
Patricia Pearson mkazi wa Burton upon Trent, alipata majeraha makubwa usoni katika ugomvi huo wa barabarani - ambao Yasin amedai alifanya katika harakati za kujilinda baada ya bibi huyo kuanza kurusha konde.
Alipatikana na hatia ya kumpiga Patricia kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Burton upon Trent mjini Staffordshire.
Mahakama ilielezwa jinsi Yasin jinsi alivyozidi kupagawa wakati akiendesha gari nyuma ya Patricia kwenye Barabara ya All Saints, Burton upon Trent majira ya saa 8 mchana wa Juni 17.
Alidai kwamba alikuwa akiendesha si zaidi ya maili 5 kwa saa kwenye barabara nyembamba ya mtaa wenye makazi ya watu, yenye matuta kadhaa kwa ajili ya kudhibiti kasi ya madereva.
Magari hayo yalipofika kwenye eneo ambapo barabara ilikuwa na nafasi, Yasin akalipita gari la Patricia na kusimama mbele yake na kuzima gari lake.
Patricia akashuka kwenye gari lake na kumfuata Yasin aliyekuwa akiendesha gari lake aina ya Peugeot 206, akainama dirishani na kumuuliza kwanini amemfanyia mfululizo wa makosa.
Bibi huyo alinyoosha mkono wake usoni kwa Yasin akijaribu kumzuia asimpige, lakini akakwepesha mkono wake na kutandika kibao bibi huyo usoni.
Patricia pia alisema kwamba Yasin alishuka kwenye gari lake na kumsukuma na kutingisha.
Lakini Yasin amekana kumpiga bibi huyo zaidi ya mara moja kama ilivyoripotiwa na mashuhuda, na kuongeza kwamba majeraha yake yanaonekana makubwa sana kutokana na umri wake.
Hukumu ya kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu.

No comments: