Tuesday, August 14, 2012

RUBANI ALIYEGUNDUA MAUAJI YA KUTISHA AENDELEA KUTESWA NA WAASI...

Wakati wa usiku, panya wanarandaranda jela kwenye nguzo za chumba cha David Simpson huku mwenyewe akiwa analala, kuoga jasho na kufungiwa kwenye hofu ya maambukizi ya malaria, akisali kuomba kwamba ndoto yake inakaribia kutimia.
Saa chache zilizopita, kijana huyu mwenye miaka 24 mtoto wa askari wa wanyamapori alikuwa na ndoto yake, kurusha ndege ndogo hadi kwenye hifadhi ya wanyama katika uwanda wa Afrika.
Sasa, akiwa katika jela ya Ngaragba karibu na Bangui katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, David bado anakabiliwa na ugumu kuamini mfululizo wa matukio yaliyomfikisha kwenye shimo la kuzimu, akituhumiwa kwa mauaji yua halaiki.
Machi mwaka huu, akiwa anafanya kazi aliyoipenda, David Simpson alifanya uvumbuzi wa kutisha mno.
Katika msitu unaofikika kwa shida sana, aliweza kugundua miili sita ya vijana iliyotenganishwa viungo ikiwa imerundikwa. Na siku iliyofuata, miili mingine saba zaidi jirani na hapo.
Vijana hao walikuwa wamefungwa pamoja na kupigwa vibaya mpaka kufa. David alifanya kile ambacho raia yeyote mwema angefanya: aliripoti tukio hilo uvumbuzi kwa mamlaka husika.
Akagundua kuwa hawezi kushangazwa na kilichotokea baadaye. Kwanza, David alikaribia kuuawa na kundi la wauaji hatari, akachapwa kwenye mateso yasiyoelezeka.
Mahema ya kampuni yake na vifaa vyake vilichomwa moto. Kisha David akatupwa jela kwa mashitaka ya kutunga ya mauaji ya halaiki ambayo aliyoyavumbua.
Juzi, akizungumza kutoka kwenye kijichumba chake kidogo na mto mwembamba, akitetemeka na huku akitokwa jasho kwenye shuka jembamba, David alizungumzia kwa kina kwa mara ya kwanza kuhusu matukio ya kutisha ambayo amepitia hadi kufikia hapo alipo sasa.
"Mara zote nilihisi Afrika ni imeathiriwa kabisa na ukatili," alisema. Lakini sasa najua kwa uhakika kwamba ni sehemu ambayo hakuna mtu anayejali kuhusu kifo."
Wakati akiongea, wafungwa wa Kiafrika walikuwa wamelala kila sehemu kuzunguka eneo alilopo kwenye vitanda vya chuma. Nje, eneo hilo limetapakaa mikojo na vinyesi kwenye kona moja.
Hakuna la zaidi kwa kifupi lenye kuhuzunisha kuona David akitetemeka kwa homa ya malaria, matundu katika chandarua yake kutokana na kutobolewa na panya, kiasi cha kushindwa kula chakula sababu ya dalili za ugonjwa huo zinazosababisha kutapika.
David alifafanua jinsi mamlaka zilivyomtaarifu kwa faragha kwmba ataachiwa huru katika siku chache zijazo, kufutiwa mashitaka yake yote.
Kwa namna ya kituko, alidhani kuwa tayari ni mtu huru wiki moja iliyopita pale waandamanaji walipovamia gereza na kuwezesha wafungwa kutoroka. Alikwenda kwenye nyumbani kwa mwajiri wake mjini humo na kujieleza yaliyomsibu, lakini Jumanne alikamatwa tena na kurudishwa ndani pamoja na wenzake wengine 18. Zaidi ya watoro 650 bado hawajapatikana.
Chini ya miguu ya David ni ukumbusho pekee anaotumaini utakaoweza kumtoa hapa. Ni popo aliyetengenezwa kwa bunda la kuni, ambalo hutumika kama silaha ya kutumainiwa na kiongozi wa wafungwa katika jengo linaloogopwa la Lollowacka ndani ya eneo hilo.
"Nilinunua kutoka kwake hivyo asingeweza kuniletea madhara zaidi. Ilitumika kuulia watu wachache," alisema David. "Kwa sasa naitumia kujikinga dhidi ya panya."
Ni maili milioni moja kutoka liliko shamba la wazazi wa David huko Gillamoor katika ukingo wa North York Moors.
Katika siku yake ya kutimiza miaka 18 tangu kuzaliwa kwake, wazazi wake wanaompenda sana, Vicky na Peter walimnunulia zawadi. Kipindi hicho alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza milango cha Sheffield, akiwafikiria uwanda wa Afrika.
Ndoto hizo ndizo zilizomfanya akaishia kufanya kazi kama rubani kwenye kampuni ya Central African Wildlife Adventures safari, ikiwa imejikita zaidi mbugani. Machi, ilikuwa ni kazi yake kwa wiki chache kusafisha njia kwenye mapori kuwezesha magari kupita kwa urahisi. Bosi wake kutoka Sweden, Erik Mararv mwenye miaka 26, alikuwa katika pori yaliko makao yao makuu huko Kocho, kusini-mashariki mwa nchi hiyo.
David na genge la wafanyakazi walipiga kambi, wakisafisha njia kwenye msitu kwa kutumia mapanga wakati wa mchana.

No comments: