Saturday, August 18, 2012

MKONGWE WA UTUNGAJI HOLLYWOOD AFARIKI DUNIA...

Mtungaji mkongwe wa Hollywood, Marvin Hamlisch, mmoja wa watu wachache duniani walioshinda Tuzo za Emmy, Grammy, Oscar na Tony, aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya ubongo wiki kadhaa kabla ya kifo chake lakini ghafla amekumbwa na tatizo la mapafu yake kushindwa kufanya kazi, kwa mujibu wa cheti chake cha kifo.
Nyaraka zilizopatikana mjini Los Angeles, ambazo zinaonesha Hamlisch alifariki kutokana na matatizo ya kupumua (mapafu kushindwa kufanya kazi kulikosababishwa na mchanganyiko wa oksijeni kushindwa kufika kwenye ubongo na shinikizo la damu.
Nyaraka zinaonesha Hamlisch alipatwa na maradhi hayo wiki kadhaa kabla ya kufikwa na mauti, hatahivyo haikufahamika kama alijijua kabla hali yake hiyo au kuonekana dalili.
Hamlisch alishinda Tuzo mbili za Academy kwa kutunga muziki katika "The Way We Were" na moja ya Oscar katika "The Sting". Pia alifanya kazi ya muziki katika "Sophie's Choice", The Spy Who Loved Me" na "A Chorus Line".

No comments: