Alidai kuwa fukara mno kiasi cha kujiunga na ghasia ili kuiba pesa kwa ajili ya chakula.
Lakini ukweli Nasir Muhsen mwenye miaka 18 alikiwa akiishi kwenye nyumba yenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 3, aliyofadhiliwa na walipakodi wa Uingereza.
Yeye na familia yake walipangishiwa nyumba moja katika eneo lenye majengo ya kisasa mjini London baada ya kutoka Irak na kudai hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza.
Taarifa za makazi ya kifahari anayoishi kijana huyo, ambayo yalikuwa ndoto kwake, sasa zimebainika baada ya juzi kuhukumiwa kifungo jela, sambamba na wenzake 15 wa genge ambalo lilihusika na kuvamia maduka na maeneo ya biashara wakati wa ghasia.
Mtuhumiwa huyo wa matukio kadhaa ni mmoja wa kundi wambalo lilifanya ugaidi katika mitaa ya Queensway na Notting Hill huko West London Agosti 8, mwaka jana, wakipora na kuchoma baiskeli moto na mabasi, na kushambulia mgahawa wa Michelin unaopendwa sana na wasanii nyota akiwamo Kate Moss.
Juzi Muhsen alifungwa miaka sita na nusu jela na Mahakama Kuu ya London kwa kile ambacho Jaji alikiita 'rekodi ya kuvutia ya uhalifu' tangu baada ya kuwasili Uingereza.
Akikenua kwa lengo la kumdharau Jaji na kucheka wakati akipelekwa jela, alitania: "Dhahiri nataka zaidi, nataka kubakia gerezani."
Gazeti la Mail limebainisha kwamba Muhsen na familia yake walitelekeza ghorofa lao lenye vyumba sita vya kulala lililoko Kensington baada ya kuwekwa hapo na halmashauri.
Ghorofa hilo ambulo kama lingepangishwa kwa bei ya sokoni lingefikia gharama ya Pauni 6,000 kwa mwezi, lilifanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kuwasili kwao mwaka jana.
Lakini wakati familia hiyo ilipotimuliwa Desemba mwaka jana kwa kushindwa kulipa malimbikizo makubwa ya kodi ya pango kwa halmashauri, lilikuwa kwenye hali mbaya sana kiasi cha wajenzi kulazimika kutumia siku kumi kufanya ukarabati.
Katika kilele cha uhalifu wao, vijana waliojifunika sura zao wakiwa wamebeba fimbo, visu na fimbo za kuchezea baseball walivamia mgahawa wa The Ledbury, wakapora wateja saa za mikononi, pesa taslimu, vito vya thamani na simu za mikononi.
Hukumu ya juzi kwa Muhsen na wenzake 15 wa kundi lake, ambao walitambuliwa na Jaji Karu kama 'kundi la mbwa' alifikisha adhabu ya jumla ya miaka 73.

No comments:
Post a Comment