Mfanyabiashara mashuhuri ambaye mwili wake uliochomwa moto uligundulika kwenye nyumba yake yenye thamani ya Pauni za Uingereza 500,000 iliyoko eneo la kijijini alishambuliwa kwa kipigo hadi kufa, polisi wamebainisha.
Mwili wa Diana Lee uligunduliwa Alhamisi iliyopita baada ya Mfanyakazi wa Posta katika kijiji cha Cranage, huko Cheshire, kubaini moto ukiendelea kuwaka kwenye gereji pembeni mwa nyumba yake kubwa iliyozungushiwa uzio.
Uchunguzi sasa umegundua kwamba mfanyabiashara huyo mwenye miaka 54 alikuwa na majeraha makubwa yaliyotokana na kipigo kwenye shambulio hilo.
Gari la mwanamke huyo aina ya Vauxhall Corsa lenye rangi ya shaba lilipatikana baadaye likiwa limechomwa moto umbali wa maili 10 kutoka kijiji cha jirani cha Mobberley.
Polisi walimkamata mpenzi wa zamani wa Diana, Neville Barrett mwenye miaka 48 ambaye alitoka na Diana Ijumaa, lakini aliachiwa kwa dhamana.
Hakuna yeyote aliyejeruhiwa kati ya paka 12 waliokuwamo kwenye majengo hayo na kwamba wamehamishiwa sehemu nyingine.
Jana Polisi wa Cheshire walisema maofisa walikuwa wakimuwinda mwendesha baiskeli aliyeonekana akitoka eneo la tukio ambako gari la marehemu lilikutwa limetelekezwa.
Pia wameomba taarifa kutoka kwa yeyote aliyeshuhudia chochote kilichotokea kwenye nyumba ya Diana katika majira ya Saa 5 asubuhi siku ya Alhamisi.
Inaaminika kwamba Diana na Barrett waliachana kufuatia mfululizo wa matukio na kwamba mwanaume huyo anaishi Hale, karibu na Altrincham.
Wapenzi hao walihamia Parklands, kitengo cha zamani cha hospitali, baada ya kununua jengo hilo mwaka 2008.
Miaka miwili baadaye walifungua sehemu hiyo ambako paka walikuwa wakilelewa katika mazingira ya starehe ikiwamo kuwekwa katika vyumba binafsi vyenye televisheni na redio.
Wapenzi hao walihojiwa gazetini ambapo walielezea jinsi paka hao wanavyovalishwa nepi kwenye jumba hilo kwa gharama ya Pauni za Uingereza 9 kwa usiku mmoja.
Askari wa zimamoto waliitwa nyumbani hapo majira ya Saa 5 asubuhi Alhamisi iliyopita baada ya Mfanyakazi wa Posta kupiga simu ya dharura. Maofisa walikagua nyumba na kukuta mwili wa Diana ukiwa umeteketea kwa moto ndani ya gereji.
Majirani wameripoti kwamba wapenzi hao walikuwa na matatizo yasiyojulikana katika siku za karibuni.
Mmoja alisema: "Hii imekuja kama mshituko kwa kila mmoja na imetufadhaisha mno. Diana alikuwa mkimya ingawa hatukuweza kumwona mara kwa mara.
Jirani mwingine alisema: "Alikuwa mwanamke mkimya lakini alikuwa na roho nzuri sana. Alifuga paka kama vile walikuwa wa kwake kabisa. Ni kitegeuchumi kikubwa sana kiasi cha kutenga vyumba vya kutosha kwa ajili yao. Hiki kilikuwa kitu kigeni kabisa hapa kwetu."

No comments:
Post a Comment