Thursday, August 16, 2012

KWA MARA YA KWANZA BINTI WA BILL CLINTON AFICHUA SIRI ZA NDOA YAKE...

KUSHOTO: Chelsea na mumewe, Marc siku ya ndoa yao. JUU: Chelsea akikumbatiwa na baba yake, Bill Clinton. CHINI: Chelsea na mama yale, Hillary wakati wa kampeni.
 Chelsea Clinton ameongea hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu ndoa yake; kumpatia mama yake 'wajukuu ambao amekuwa akiwahitaji'; na kuungana na wazazi wake katika siasa.
Akiwa na umri wa miaka 32, na maarufu kwa kuweza kuficha siri za maisha yake binafsi, binti huyo wa Bill na Hillary Clinton alikuwa kimya kwa kipindi kirefu kuhusu mahusiano yake na mumewe, Marc Mezvinsky lakini katika mahojiano mapya, wawili hao walijadili kwa uwazi maisha yao ya baadaye.
Katika toleo la Septemba la Jarida la Vogue, alikiri kuhitaji watoto 'katika miaka kadhaa ijayo, kwa imani…mapenzi ya Mungu".
Mwaka jana kulizagaa ripoti kwamba ndoa ya wawili hao ilikuwa kwenye matatizo, zikishikilia ukweli kwamba Marc, mfanyakazi wa benki, alipanga nyumba huko West 'kwa ajili ya mchezo wa kuserereka kwenye barafu' baada ya kuacha kazi kwenye benki ya 3G Capital.
Waandishi wa habari walikusanyika nje ya nyumba yao, na kwa miaka miwili iliyopita, watu wameendelea kuhoji kama wanandoa hao wataachana.
Mkuu wa wafanyakazi wa nyumba yao, Bari Lurie alisema: "Hakuna lolote kati ya hayo lililo la kweli.
"Lakini kinachosababisha hayo yote kwao ni kwamba habari zimekuwa zikiandikwa sababu hakuna yeyote kati yetu anayetilia maanani. Ilikuwa ni somo la kutufumbua macho. Chelsea amebaini, "Pengine natakiwa kutoka nje na kujipambanua japo kidogo", alisema.
Wawili hao walikutana mwaka 1992 katika shughuli za kila mara ambazo Clinton alikuwa akihudhuria katika miaka aliyokuwa Ikulu, wakati huo Chelsea akiwa na miaka 12 tu, wakati Marc akiwa na miaka 15.
Wakati wakibaki kuwa marafiki wakiwa mbalimbali, ilikuwa baada ya Chelsea kujiunga na Chuo Kikuu cha Stanford, ambapo mumewe mtarajiwa alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili, ndipo urafiki wao ulipogeuka kitu kingine zaidi.
Dhahiri, mahusiano yao yalibaki siri hadi pale Chelsea alipoachana na rafiki yake wa kiume wa siku nyingi kutoka Oxford, Ian Klaus.
Lurie alieleza: "Chelsea alimtumia Marc kama bega kuweza kufanikiwa kimasomo."
Wakati wa mahojiano, Chelsea alibainisha jinsi mama yake asivyo na subira kuhusu suala la wajukuu.
Alikiri: "Hili limekuwa jambo ambalo Marc na mimi tumekuwa tukiliongelea sana. Mara zote nilitambua kwamba mini ni kiungo cha maisha ya wazazi wangu pale nilipokuwa nikikua. Na ninadhamiria kwamba watoto wetu watajihisi hivyo pia.
"Marc na mimi wote pamoja sasa tunafanya kazi kwa bidii sana, lakini nadhani katika miaka kadhaa, naamini…mapenzi ya Mungu. Na ninaamini mama yangu atasubiri hadi wakati huo."
Hillary alikuwa na miaka 32, umri wa binti yake sasa, pale alipobeba ujauzito wa Chelsea Februari, 1980, baada ya kuwa 'first lady' wa Arkansas, na mwanamke wa kwanza kufanywa mshirika kamili katika Kampuni ya Rose Law Firm, ambako alikiwa akivuna pesa zaidi ya mumewe.
"Ingawa anataka kuweka alama kubwa juu ya dunia kabla ya kuwa mama, Chelsea pia alijadili uwezekano wa kuwafuata wazazi wake katika siasa.
Alisema: "Kabla mama yangu hajaanza kampeni ningeweza kusema hapana. Na sasa sifahamu…"
Chelsea alitawala vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali pale alipofunga ndoa na Marc mwaka 2010, katika sherehe iliyofana sana ambayo inakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 3.

No comments: