Wazee wawili wajane walikuwa na urafiki kwa miaka mitano. Hatimaye Babu akaamua kumweleza Bibi nia yake ya kutaka kumuoa. Bibi kwa haraka akajibu, "Sawa, niko tayari!"
Kesho yake asubuhi alipoamka, Babu hakuweza kukumbuka alijibiwa nini na Bibi jana yake kuhusu kutaka kumuoa. Akaanza kujiuliza, "Hivi alikuwa na furaha? Nadhani, ngoja, hapana, alinichekea…"
Baada ya kama saa moja akijaribu kukumbuka bila mafanikio, akaamua kumpigia simu Bibi. "Haloo, mwenzako nimechanganyikiwa hapa, sikumbuki ulinijibu nini kuhusu maombi yangu ya kutaka kukuoa."
Bibi akajibu, "Ooh, nimefurahi umenipigia. Nakumbuka nilimjibu mtu fulani 'Sawa, niko tayari'. Lakini sikumbuki alikuwa nani?" Kasheshe...

No comments:
Post a Comment