Sunday, August 26, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa akiwa anakatiza vichochoro kuelekea kwake Kinondoni Mkwajuni kakutana na vibaka na kuanza kupambana nao ili wasimwibie. Baada ya patashika ya kama dakika kumi hivi, vibaka wakamshinda nguvu na kufanikiwa kumpora pochi yake na kutokomea gizani huku jamaa akiwa hoi chini. Dakika tano baadaye vibaka wakarejea eneo lile na kumfokea yule jamaa, "Yani vurugu zote zile kumbe pochi ina Shilingi Mia Tano tu!" Jamaa kwa sauti ya uchovu akajibu, "Ilibidi nipambane ili msiweze kuzipata Shilingi Laki Moja nilizoficha kwenye kiatu!" Ebo...

No comments: