Thursday, August 16, 2012

BOBBY BROWN AANZA TIBA KUACHANA NA ULEVI...

Bobby Brown kwa sasa anaendelea kupata tiba dhidi ya ulevi wa kupindukia, imefahamika.
Vyanzo vya habari vilivyo karibu na Bobby vimeeleza kuwa mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la New Edition amekubali mwenyewe kupatiwa tiba hiyo haraka iwezekanavyo sababu 'amegundua asingeweza kufanya hivyo mwenyewe.'
Imeelezwa kwamba amekuwa akipata tiba ya matukio yanayosababishwa na matumizi ya pombe, tatizo ambalo Bobby amekuwa akisumbuliwa nalo kwa miaka mingi.
Vyanzo vimeongeza, Bobby "aliamua kwamba anahitaji msaada na kutaka kwa dhati kabisa kuondokana na matatizo hayo kwa ajili ya mustakabali wa watoto wake."
Bobby alikamatwa kutokana na kuendesha gari huku akiwa amelewa Machi mwaka huu, mwezi mmoja baada ya mpenzi wake wa zamani Whitney Houston kufariki.

No comments: